Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE HEMED SULEIMAN ABDULLA AKIKAGUA UWANJA WA MICHEZO WA AMAANI MJINI ZANZIBAR
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema kukamilika kwa Uwanja wa Michezo wa Amaani utatoa nafasi kwa Nchi mbali mbali Dunia kuweza kuutumia Uwanja huo utakaokuwa Uwanja wa kisasa uliokidhi Viwango vyote vya Kimataifa.
Ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendelea ya Ujenzi wa Kiwanja hicho uliopo katika hatua za mwisho kuweza kukamika.
Mhe Hemed amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi kwa maono yake makubwa na nia thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar kwa kuamua kuujenga upya Uwanja wa Amaani ili kuwawezesha wanamichezo wa Zanzibar na nje ya Zanzibar kucheza katika viwanja vyenye mandhari nzuri na hadhi ya Kimataifa.
Aidha Mhe. Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Serikali inaimani kubwa na kampuni ya ORKUN inayojenga Uwanja huo na kuutaka uongozi wa kampuni hio kukamilisha ujenzi kwa wakati na kiwango kilichokusudiwa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amewataka wakandarasi na Mshuri elekezi wa Mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi kwa kufanya kazi Usiku na Mchana na kwa uwaminifu mkubwa ili Ujenzi huo ukamilike kwa wakati na kwa kiwango kilichokusudiwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vya baadae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Ujenzi wa Uwanja huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayowataka Viongozi kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazoendana na wakati ikiwemo michezo .
Sambamba na hayo Mhe Hemed amesema Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Amani kama alivyoahidi Mhe Rais wa Zanzibar Dkt Hussen Ali Mwinyi ili kutoa fursa kwa wanachi wengi kuweza kushiriki katika sherehe hizo pamoja na kujionea kile kilichofanywa na serikali ya awamu ya Nane (8).
Amewataka waandishi wa habari kutangaza mazuri na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi ambayo imedhamiria kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wake.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Bi. Fatma Hamad Rajab amesema Uwanja wa Amaani umejengwa kwa kufuata Vigezo vya Kimataifa na matakwa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambao unatarajiwa kuchukuwa watazamaji elfu kumi na Sita (16,000) na kutoa fursa kwa Timu za ndani na nje ya nchi kuutumia Uwanja huo.
Amefahamisha kuwa Uwanja wa Amaani unajumuuisha Viwanja vya mpira wa miguu vya kisasa, uwanja wa Netball, Basket ball, Handball, Ukumbi wa Judo, Indows Game na Hoteli ambayo itasaidia kutoa huduma ya makaazi ya wageni watakaotoka nje ya Zanzibar.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa amesema Serikali ya Mkoa itahakikisha inatembelea mara kwa mara katika uwanja huo na kuhakikisha amani inatawala katika kiwanja hicho ambacho Serikali imewekeza fedha nyingi kwa maslahi ya Taifa.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.