MLEZI WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA WAZEE,MACHIFU NA WATU MAARUFU
Naibu katibu Mkuu wa CCM bara na Mlezi wa Mkoa wa Mbeya Ndg. Anamringi Macha leo tarehe 9 Oktoba amekutana na Wazee maarufu na Machifu wa Mkoa wa Mbeya katika ukumbi wa CCM Mbeya Mjini,
Naibu Katibu Mkuu Macha amesema Chama kitaendelea kuenzi,kulinda na kuheshimu kundi la Wazee kwani ndiyo chimbuko la maendeleo yaliyofikiwa hivi sasa ndani ya Chama na Taifa kwaujumla.
Macha, amesema kikao chake hicho ni cha kujitambulisha kama Mlezi wa Mkoa huo kukutana na wazee hao kwa lengo la kusikiliza ushauri,maoni na mapendekezo yao ili yaweze kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulezi wa Mkoa.