SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, IMEIPONGEZA MAMKAKA YA MAPATO ZANZIBAR (ZRA) KWA JITIHADA ZA KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATO NCHINI HASA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.
Pia Serikali imetoa pongezi hizo kwa kufanikiwa kuvuka lengo la makusanyo ya kodi zaidi yaliyowekwa kila mwezi na kuwa na ukuaji mzuri wa mapato ikilinganishwa na mwaka jana. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameyasema hayo ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi, kwenye sherehe za kilele za mwezi wa Shukurani na furaha kwa walipa kodi wa Zanzibar.
Alisema, kwa kipindi cha miezi mitano (5) kutoka Julai hadi Novemba 2023, ZRA ilikadiriwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 276.063 na imefanikiwa kukusanya makusanyo halisi shilingi bilioni 288.251, sawa na ufanisi wa asilimia 104.42. hivyo, kufanikiwa kuongeza ukusanyaji mapato kwa asilimia 21.93 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi bilioni 236.407 ya kipindi kama hicho cha mwaka jana.
Alisema, hali hiyo inajenga imani ya uwezekano wa kukusanya mapato zaidi na zaidi. Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwataka wafanyakazi wa ZRA, kufanyakazi ya ukusanyaji wa mapato kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili waepukane na vishawishi kutoka kwa wafanyabiashara wachache wasiokuwa waadilifu.
Pia, alitoa indhari na kueleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mfanyakazi yeyote wa ZRA na TRA Zanzibar, atayekwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Alionya, mfanyakazi yeyote atakaebainika kukwepesha mapato ya Serikali, hatua kali za kiutumishi na kijinai zitachukuliwa dhidi yake. Katika hali nyengine Rais Dk. Mwinyi aliwaahidi watumishi wa ZRA kuwa Serikali itaendelea kuyaangalia maslahi yao kama walivyoangaliwa wafanyakazi wengine wa Serikali ili kuongeza hamasa ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kuiwezesha ZRA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
Hivyo, Dk. Mwinyi aliziagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi washirikiane na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, kukamilisha marekebisho stahiki ya mishahara ya watumishi wa ZRA, ili wapate faraja na waendelee na ufanisi katika kazi zao.
Kwa upande wa wafanyabiashara wote waliopo Zanzibar na wanaokuja kuwekeza, Dk. Mwinyi aliwahakikishia kwamba Serikali imeimarisha mfumo wa kodi iliyo rafiki itakayorahisisha biashara kwa kuimarisha mfumo wa kodi ulio sawa kwa kila mfanyabiashara. “Hakuna atakayependelewa wala kuonewa. Tutaendelea kuimarisha mfumo wa kodi ulio rahisi kuutumia (convenient) kwa kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya kidigitali na kuwafikia walipakodi wengi zaidi kwa kuimarisha Ofisi za kodi” Dk.Mwinyi, aliwahakikikisha wafanyabiashara hao.
Vile vile Rais Dk. Mwinyi, aliitaka mikoa na wilaya zote nchini kuendelea kuimarisha mfumo wa kodi unaotabirika (certainty) kwa kuendelea kutoa elimu ya kodi ili kila mfanyabiashara ajue aina ya kodi anayostahiki kulipa kwa wakati husika. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, akizungumza kwenye hafla hiyo alisema, kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Maendeleo makubwa yamefikiwa kutokanana ukusanyaji mzuri wa mapato yaliyosaidia kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya maendeleo.
Alisema Maendeleo hayahitaji vikwazo, ufinyu wa Maendeleo unatokana na kukosa maono, alieleza Zanzibar imejifunza utayari kutoka kwa Rais Dk. Mwinyi wakitafakari zaidi bila kuweka vikwanzo vya Maendeleo. Alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa nchini ni jitihada za Mhe. Rais Dk. Mwinyi kushajihisha ulipaji bora wa kodi za kielektroniki. Naye, Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya ZRA, Prof. Hemed Rashid Hikmany, alieleza miongozi mwa majukumu ya bodi hiyo ni kuhakikisha wanafanyakazi
wanafanyakazi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa hiari, kuhakikisha wanafanyakazi kwa ukaribu na weledi ili kufikia malengo ya Serikali ya ukusanyaji bora wa mapato.
Kamishna Mkuu wa ZRA, Yussuf Juma Mwenda naye alieleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na ZRA ikiwemo kushajihisha walipakodi kwa ufanisi kupitia mfumo wa kisasa wa ZIDRAS unaowarahisishia walipakodi wa aina zote, wakubwa, wakati hadi wadogo kulipakodi na kurejesha marejesho ya kodi (returns) kwa wakati kupitia teknolojia ya kisasa. Alisema, ZRA pia imefanikiwa kutoka makusanyo ya Shilingi bilioni 565 kwa mwaka jana ikilinganishwa na bilioni 374 za kipindi kilichopita.
Pia alieleza ZRA imeanza kuchukuakoti za majengo ya ghorofa ikiwemo mahoteli ambao wamekuwa na mwitikio mkubwa kwa serikali, alisema nyumba ndogo hazihusiki na kodi hiyo.
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
30-05-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
30-05-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026