Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


HAPI APOKELEWA KIBAHA VIJIJINI AWAONYA VIONGOZI WASIOWAJIBIKA  ATAKA WASILAUMU CHAMA

alternative

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu. Ally Salum Hapi (MNEC) akiwa Kibaha Vijijini amepigilia msumari suala la viongozi waliopo madarakani kuhakikisha wanafanya kazi na kutoa mrejesho kwa wananchi waliompatia madaraka hayo kuwaongoza hususani katika kipindi hiki ambacho wataingia katika kugombea nafasi zao na kuomba ridhaa kwa wananchi kuwachagua badala ya kuja kulalamika baada ya kushindwa katika chaguzi.

Hapi alisema katika wakati huu ambao wanaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa chama hakitaunga mkono wagombea wasiotokana na wananchi ambao watakuwa na wakati mgumu katika kuwatafutia kura 

"Hatutaki wagombea wa kuunga unga, tunataka mgombea ambaye wananchi watahitaji awaongoze na ndiyo tutashinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao" alisema Hapi

Hapi amewataka wanaccm na viongozi kujenga utaratibu wa kukaa katika vikao kutatua changamoto zinazowakabili kwa kufuata utaratibu uliowekwa na chama cha mapinduzi 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani Mwishehe Mlao amewanyoshea kidole wale wote wanaoendelea kusababisha mivutano ndani ya chama hicho na kufanya wananchi wasikipende chama huku mwenyekiti wa chama wilaya ya Kibaha vijijini akisema hakuna migogoro bali ni jeuri ya baadhi ya wanaccm.

alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi