Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS SAMIA KUJA NA "PROGRAM" YA KUSIKILIZA MWANANCHI MMOJA MMOJA.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan ametangaza kutenga siku moja kila mwezi ili kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za mwananchi mmoja mmoja.
Hatua hii imetangazwa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Ndg. Paul Makonda wakati akizungumza na wanahabari kwenye Ofisi Ndogo za CCM jijini Dar es Salaam.
"Hatua ya Rais inakuja ili kudhihirisha kwa vitendo tamanio lake la kuwataka watendaji wa serikali kutenga muda zaidi kusikiliza wananchi na kutatua kero zao mbalimbali." asema Makonda.
Sambamba na hayo CCM imewaelekeza viongozi wote wa serikali kutatua changamoto za wananchi kwa wakati kwakua kutofanya hivyo ni kuwachonganisha na Serikali yao.
"Maelekezo ya CCM kwa kila aliye na nafasi katika uongozi wa serikali ana wajibu wa kutatua changamoto za wananchi na afahamu kuwa ofisi si yake bali ni ya umma, kutotatua changamoto za wananchi ni kuwafanya wananchi kuichukia serikali yao na kukichukia Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan." asema Makonda.
Pia, Makonda ametoa tathmini ya ziara mikoani ambapo hadi kufikia sasa Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo imefika mikoa 23 na kufanya mikutano 247 na kukutana na changamoto zaidi ya 2000.
"CCM tunawashukuru sana waandishi wa habari kwa namna ambavyo mmekuwa bega kwa bega kuhabarisha umma juu ya mambo mengi mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayotokana na chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mwenyekiti na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan."
Ndg. Paul Makonda amefanya Mkutano na waandishi wa habari leo Machi 5, 2024 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.