Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja kuongeza bidii na maarifa kwenye masomo yao ili kutoa ufaulu mzuri kwa ustawi wa maendeleo ya maisha yao ya baadae.

alternative

Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini, Unguja kwenye hafla ya kuwagaia wanafunzi wa kike taulo za hedhi Salama. Alisema, hakuna linaloshindikana endapo wataongeza bidii ya masomo yao ili waepukane na unyanyasaji kwenye jamii zao.

Mama Mariam Mwinyi alieleza mradi wa ‘Tumaini initiative’ wa ZMBF unaotoa taulo za hedhi salama, umelenga kufufua ndoto wa wasichana na wanafunzi wa kike kuendelea kuhudhuria masomo yao kila mwezi bila kukatisha masomo yao hasa wanapokua kwenye ada zao za kila mwezi.

Aidha, alieleza taulo hizo zitawapunguzia mzigo wa gharama za matumzi ya kila mwezi wazazi nawalezi wa wanafunzi hao kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano endapo zitatunzwa vizuri pamoja na kuwaweka sakama na afya njema kwani hazina kemikali. Alisema mbali na kutunza afya za wasichana na wanafunzi hao lakini pia kutunza mazingira kwa kukwepa kutupa taulo ovyo badala zake wazifue na kuzitunza vizuri. Hivyo, aliomba wafadhali zaidi kujitokeza kuufadhili mradi wa ‘Tumaini initiative’ ili kuwaondoshea mzigo mzito wa uchumi wananfunzi na wazazi kuepuka gharama kubwa ya kutumia taula za kutupa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Fatma Fungo alisema lengo la taasisi hiyo ni kuwafikia zaidi ya wanafunzi 20,000 ndani ya muda mfupi kwa kuwapa taulo za hedhi salama ambapo kwa kipindi cha miezi minne tayari wamewafikia wanafunzi 1557 wa skuli mbalimbali za Unguja Pemba.

Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mahmoud, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Sadifa Juma Khamis alieleza masikitiko yake ya matokeo mabaya ya Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe, hivyo aliitoa wito kwa walimu na wanafunzi wa Skuli hiyo kuongeza jitihada ili kuibadilisha hali iliyoposasa kwa kuleta mabadiliko makubwa na matokeo ya mitihani yao ya Taifa.

Naye, Mkurugenzi Secondari, Bi Asya Iddi Issa aliwahimiza wanafunzi hao usafi wa afya zao na mazingira wanayosomea hasa kwenye matumizi ya taulo hizo ili kupata muda mzuri wa kujisomea. Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wajamama, inayojishughulisha na kutoa taaluma ya afya ya uzazi, Dk. Mwanakheir Mahmoud alisema 48% ya wasichana na wanafunzi wa kike hushindwa kuhudhuria masomo yao ipasavyo Kila mwenzi kutokana na kutokua na hedhi Salama, aidha alieleza asilimia 28 ya wasichana hawana maarifa ya kujitunza na kutumia hedhi salama.

Alisema mbali na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa jamii lakini pia wamekusudia kuwafikia zaidi ya wasichana 500 kuwapa elimu ya hedhi salama. Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) iliasisiwa Julai mwaka 2022 na kuzinduliwa rasmi Febuari mwaka jana, mwezi Machi mwaka huu, ilizindua Mpango Mkakati wa miaka mitatu pamoja na mradi wa “Tumaini kit” ambao hadi sasa umefanikiwa kuzalisha taulo za kike zaidi ya 5000 na kuzisambaza zaidi ya 1500 kwa wanafunzi na wasichana wa skuli za msingi na sekondari kwa Unguja na Pemba.

Aidha, taasisi hiyo inafanya kazi kwa karibu na tasisi za Serikali zikiwemo Mahakama ya Zanzibar, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Uchumi wa Buluu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Wazee na watoto, Wizara ya Habari na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi