DK.MWINYI ASEMA SERIKALI ITAWEKA MIUNDOMBINU BORA KWA MICHEZO YOTE ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na mwenye kiti wa baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaweka miundombinu bora kwa michezo yote Zanzibar.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la Msingi viwanja vya nje vya Amani vitakavyojumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mmpira wa meza, netiboli, mpira wa wavu, mpira wa vivyoya, mpira wa kikapu, mpira wa mikono, mchezo wa judo, michezo ya ngumi ikiwemo masumbwi, jujistsu, taekwondo na karate.