COMRADE MONGELLA AWASILI KAHAMA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, amewasili mjini Kahama leo, tarehe 7 Septemba 2024, kwa ziara ya siku moja wilayani humo. Ziara hii inalenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama ya 2020-2024. Mongella pia amekutana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kahama kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa kazi za chama. Ziara yake mkoani hapa inatarajiwa kudumu kwa siku saba.