Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RABIA: MRADI WA KUSINDIKA, KUCHAKATA GESI ASILIA UTAIFUNGUA LINDI KWA MAENDELEO
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid, amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa mradi wa kuchakata gesi (LNG) kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza mkoani Lindi Julai 30, 2024, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi aliyeongozana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti mkoani Lindi, Rabia amesema kuwa mchakato wa utekelezaji wa mradi huo unaendelea.
Rabia amesema kuwa utekelezaji wa mradi LNG ni maelekezo na ahadi ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2024 na kwamba mwakani hatua mbalimbali zitafikiwa ikiwamo kutia saini mikataba ya utekelezaji huo.
Aidha, amesema kuwa kuanza kwa mradi huo kutazalisha ajira nyingi za kudumu na za muda mfupi kwa wakazi wa Lindi na mkoa huo utaendelea kupata maendeleo kupitia mauzo ya bidhaa na huduma mbalimbali wakati wa utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya sh. trilioni 70.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.