Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
DK MWINYI AZIKARIBISHA TIMU ZA KIMATAIFA ZANZIBAR KUJA KUJIONEA HAIBA MANDHARI NZURI NA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO
Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na timu ya “Kaizer Chief” kutoka Afrika Kusini iliyoalikwa nchini ya timu ya Wananchi “Yaung Aficans”, Yanga. Alisema, Zanzibar ni kisiwa cha utalii chenye vivutio vingi vya Fukwe za bahari na
Hifadhi ya kimataifa ya Mji Mkongwe, hivyo aliikaribisha timu ya “Kaizer Chiefs” kuitumia fursa ya uwepo wao nchini kutembelea baadhi ya vivutio hivyo ili wakawe mabalozi wazuri wanapokuwa nchini kwao. Aliwataka wanapopata tena fursa warudi nchini kuitembelea zaidi Zanzibar pia waitangaze sana wanapokuwa Afrika ya Kusini na mataifa mengine kwa ujumla kupitia utalii wa michezo. Rais Dk. Mwinyi alisema, Zanzibar imekua na ndoto kubwa ya kufanya utalii wa michezo, hivyo ujio wa Kaizer Chief umeakisi dhana halisi ya sekta ya Utalii nchini. Vile vile Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza Kaizer Chief aliyoambatana na ujumbe wa watu 58 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu hiyo, kwamba Zanzibar ina maeneo mazuri ya kupumzikia hivyo, aliwaeleza kuitumia Zanzibar kwajili ya mapumziko yao na familia zao pia kuitangaza kimataifa kwa kutaja mazuri ya utalii waliyoyashuhudia
.Naye, Waziri wa Habari Vijana na Michezo, Tabia Mauli Mwita aliushukuru uongozi wa timu ya Yanga kwa juhudi zao za kuikaribisha nchini, timu ya Kaizer
Chief sambamba na kumueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba ujio wa timu ya Afrika Kusini nchini ni kuendeleza jitihada za kuutangaza utalii wa nchi. Pia, Waziri Tabia alimuarifu Dk. Mwinyi mwamba, ameikabidhi bendera ya taifa timu ya wanawake ya Zanzibar, chini ya umri wa miaka 18 kwenda Tanzania Bara kuiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya Cecafa yanayofanyika Tanzania Bara wakizishirikisha nchi mbalimbali kutoka Afrika, ikiwemo Tanzania, Burundi, Rwanda na Ethiopia. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa timu ya Yanga, Injinia Hersi Ally Said alisifu juhudi zinazofanywa na Rais Dk. Mwinyi kuitangaza nchi kiutalii kimataifa,pamoja na kukuza utalii. Alisema, hatua ya kuifikisha timu ya Kaizer Chini, Zanzibar ni kuunga mkono juhudi zake na kuitangaza Zanzibar kimataifa na kuongeza taarifa za uwepo wa timu hiyo kisiwani Unguja hazitosambaa Afrika Kusini pekee bali na mataifa mengine ya dunia. “Hatua ya kuileta Zanzibar, Timu ya Kaizer Chiefs, yenye historia barani Afrika ni sababu ya kuitangaza Zanzibar kimataifa na kufungua milango kwa wageni wengine kuja kutembelea vivutio vya utalii vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla”alieleza Hersi. Alisema anaimani kubwa na Kaizer Chiefs, kwamba ikiondoka nchini itakua imeitangaza zaidi Zanzibar Kimataifa kupitia mashabiki wao wa Afrika ya Kusini namataifa mengine ya dunia.Pia, Injinia Hersi alimueleza Rais Mwinyi kwamba timu ya Yanga imekua ikishiriki mashindano ya muhimu ya Mapinduzi Cup yanayofanyika Zanzibar na kuahidi kwamba timu hiyo imejipanga kwa kikosi maalumu kushiriki tena mashindanoyajayo.Alieleza, ujio wa mabingwa hao kutoka Afrika kusini “Kaizer Chief” ni heshima kubwa nchini pia kuitembelea Zanzibar, alisema ugeni huo ulikwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya wananchi ilivyofanikisha kuwapokea wageni kufuatia mwaliko waliowatumia na kuongeza kuwa wiki ya wananchi kwa timu yao ya Yanga iliyoanza Julai 15 na kuhitimishwa Julai 22 mwaka huu.
Timu ya Afrika Kusini Kaizer Chief ilifanikiwa kutembelea maeneo machache ya Zanzibar kujionnea utajiri na uzuri wa haiba ya Kisiwa cha Unguja.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.