Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ HUSSEIN MWINYI AMEHIMIZA JAMII KUENDELEA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO ILI KUJENGA TAIFA LA MAENDELEO NA UCHUMI
Al hajj Dk. Mwinyi, alitoa nasaha hizo kwenye Msikiti wa Ijumaa Miembeni Mkoa wa Mjini Magharibi, alikojumuika pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa. Rais, Al hajj Mwinyi, aliieleza jamii kadri inavyokusanyika pamoja kwenye shughuli mbalimbali za maisha ya kila siku, wasichoke kuhimizana umuhimu wa amani ya nchi, kwani kufanya hivyo ni kutimiza malengo mazuri waliyoyakusudia ya ustawi wa jamii bora na maendeleo ya uchumi. “Haya yote tunayoyafanya, yawe ya maendeleo, jamii au ibada misikitini yanategemea amani ya nchi” Alisisitiza Al hajj Dk. Mwinyi. Al hajj Dk. Mwinyi alieleza umoja na mshikamano wa jamii ndio msingi wa kufikia malengo iliyojiwekea, kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar”. Hata hivyo, aliwataka waumini hao waendelee kuombeana du’a na kuliombea taifa katika kufanikisha maleongo yake. Akihutubu kwenye sala hiyo, Khatibu Sheikh Khalid Ali Mfaume alieleza umuhimu wa siku ya Ashura kwenye historia ya uislam na kusisitiza jamii ya waislam
kuendelea kukithirisha ibada hasa kwenye mwezi mtukufu wa Muharam.Sheikh Khalid ambae pia ni Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, alisema, Mwezi wa Mfunguo nne (Muharami) ni miongoni mwa miezi minne mitukufu ya Mwenyezi Mungu kwenye kalenda ya uislam pia alieleza mwezi 10 Muharam ni sunna kufunga funga ya Ashura kwa waumini wa dini ya kiislam. Alisema, funga hiyo ni bora baada ya Ramadhani ambayo Mtume (SAW) aliifunga mara baada ya kuhamia Madina.
Hivyo, aliihimiza jamii ya waislam kuzitumia vyema siku tukufu za mwezi wa Muharam kwa kuendelea kukithirisha ibada na kuacha mabaya yote aliyoyakata Mwenyezi Mungu (S.W).
Mara baada ya sala ya Ijuma, Rais Al hajj Dk. Mwinyi alimtembelea kwa kumjuulia hali Bi. Khadija Abass Rashid, mkaazi wa Rahaleo Wilaya ya Mjini alieshiriki kwenye tukio la historia la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 wakati wa kuasisiwa kwa taifa la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.