Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA YA NSALAGA - IFISI (KM 29) KWA KIWANGO CHA LAMI MKOANI MBEYA - MWENEZI MAKALLA

alternative

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Taifa Ndugu. Amos Makalla amesema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amedhamiria kufanya upanuzi wa ujenzi wa barabara kwa njia nne ya Nsalaga hadi Ifisi yenye urefu wa Kilomita 29 kwa kiwango cha lami.

Akizungumza na Mabalozi wa mashina, viongozi wa serikali, wazee, machifu na vingozi wa dini pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo, Mwenezi Makalla amesema kuwa upanuzi wa barabara hiyo utaharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Jiji la Mbeya na maeneo jirani na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji.

Makalla amesema utekelezaji wa mradi huo ni mkakati wa Rais Dkt. Samia kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari.

 Ujenzi huo unafadhiliwa na serikali kwa 100% ambao utagharimu kiasi cha Tsh Bilioni 138.7 ambapo mkandarasi ni kampuni ya CHICO .

Makalla amesisitiza kuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia ni kujenga barabara hiyo ambayo inaanzia Igawa - Songwe - Tunduma (urefu wa km 218) na kuunganisha mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe na Nchi jirani za SADC kupitia Zambia, Malawi na Congo ambapo lengo pia ni kuimarisha na kuboresha ushirikiano wa kibiashara.

" Mbeya imepiga hatua kubwa ya maendeleo, biashara na uwekezaji umeongezeka ndani ya mbeya, hatua hizi kubwa ni kutokana na utulivu na kama jina la Tulia ndio utulivu basi hakika mmepatia ."

" Tusirudie makosa ya miaka ya nyuma, tunahitaji utulivu na watu kuendelea na shughuli zao za maendeleo "

" Unakuta mtu anasema mbeya hakuna maendeleo, sasa kwani maendeleo ni ya kuyatafuta si yanaonekana..mfano kwasasa usafiri wa anga ni muda wote hapa Mbeya lakini unakuta mtu anajifanya haoni na anatumia usafiri wa anga hapa Mbeya kila kukicha ."

" Kazi yetu wana CCM ni kuyasemea mazuri yaliyofanywa na serikali yetu, tusiwaachei watu wengine kwakuwa chama chochote cha siasa dunia ndicho kinachofanya kazi ya kuomba ridhaa kwa wananchi na kikichaguliwa kinaenda kuunda serikali kwahiyo tembeen kifua mbele bila uoga kueleza mafanikio ya CCM "

πŸ—“οΈ17 Aprili, 2024
πŸ“Jijini Mbeya

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine