Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Awamu ya Nane(8) inayoongozwa na Rais Dkt Hussen Mwinyi itaendelea kutatua chamgamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi kwa kuwaletea maendeleo endelevu mijini na vijini.
Ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbali mbali inayojengwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarr ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu mbali mbali ikiwemo ya Elimu na masoko ili wanafunzi waweze kusoma katika skuli zenye hadhi na zinazokidhi mahitaji ya kusomea na kufundishia sambamba na wananchi waweze kufanya biashara zao katika masoko ya kisasa yatakayokidhi mahitaji ya wananchi.
Amesema kuwa kuwepo kwa miundombinu bora ya elimu ikiwemo Skuli za ghorofa zenye dakhalia na nyumba za kuishi walimu karibu na skuli hizo zitasaidia wanafunzi kusoma kwa utulivu na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kila mwaka.
Aidha Mhe.Hemed amewataka wafanyabiashara kufuata uataratibu ambao utaandaliwa na viongozi husika pindi yatakapo malizika na kuhamia katika masoko hayo sambamba na kuwataka kuyatunza na kudumisha usafi na kuachana na tabia ya kufanya bishara nje ya soko jambo ambalo linapelekea uchafuzi wa mazingira na kuondoa haiba ya masoko hayo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza wakandarasi wa ujenzi wa miradi hio kuongeza kasi ya ujenzi ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwasisitiza kujenga kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili majengo hayo yaweze kudumu kwa muda mrefu.
Sambamba na hayo Mhe.Hemed amewataka Viongozi kuendelea kuwafahamisha wananchi yale yote mazuri ya maendeleo nayofanywa na Rais Dkt. Mwinyi yanayowanufaisha wananchi wote wa Zanzibar pasipo na ubaguzi wa aina yoyote.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wakuu wa nchi sambamba na kuwataka kuendelea kuitunza Amani iliyopo nchini ambayo ndio chachu ya maendeleo.
Kwaupande wao mawaziri wenye dhamana ya kusimamia ujenzi wa miradi hio wamesema ziara za Mhe. Makamo wa Pili wa Rais zinatoa msukumo na kuamsha ari ya kutekeleza majukumu yao ya kuisimamia miradi hio ili iweze kukamiliaka kwa wakati na kiwango kilichokusudiwa.
Mawaziri hao wamemuhakikishia Mhe. Makamo wa Pili wa Rais kwamba miradi hio itamalizika kwa wakati uliopangwa na kwa viwango vya hali ya juu ili iweze kuwanufaisha wananchi kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoelekeza.
Nao wakandarasi wanaojenga miradi hio wamesema baadhi ya maeneo wanayojenga wamekuwa wakikumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo changamoto ya umeme mdogo na ubovu wa miundombinu ya barabara inayopelekea vinapunguza kasi ya ufanyajikazi kwa kukosa nyezo muhimu za kujengea.
Aidha Wakandarasi hao wameahidi kukamilisha miradi hio kwa wakti uliopangwa na kwa viwango bora kama walivyokunaliqna.
Katika ziara hio Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekagua mradi wa ujenzi wa SOKO LA CHAANI, UJENZI WA SKULI YA SOKONDARI, DAKHALIA NA NYUMBA YA WALIMU iliyopo GAMBA, UJENZI WA SOKO LA MKWAJUNI NA na UJENZI WA SKULI YA SEKONDARI MKOKOTONI.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.