Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS WA JMT DKT. SAMIA AMEONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KUTOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA HESHIMA YA MWISHO KWA HAYATI MZEE ALI HASSAN MWINYI.

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Rais Mstaafu wa Zanzibar  na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi  katika Uwanja  wa Amani, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja  tarehe 2 Machi 2024.

Pia Rais Dkt. Samia ameongoza  Viongozi mbalimbali kutoa salamu za rambirambi  na pole kwa watanzania na familia ya Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja huo. 

Viongozi mbalimbali wameshiriki wakiwemo wa Serikali ya  SMT na SMZ,  wa Vyama vya siasa, Vyombo vya ulinzi na usalama, Dini, Waheshimiwa Mabalozi pia wawakilishi wa nje ya Tanzania wakiwemo  Namibia, Burundi na Comoro walitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Nchi zao.

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi