Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, ametoa uchambuzi wa kina kuhusu ushindi mkubwa wa chama hicho katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Septemba 27, mwaka 2024
Dkt. Dimwa ameleza sababu, dhamira na mafanikio yaliyofikiwa na CCM, na pia kuonyesha jinsi ushindi huo unavyotoa picha ya nguvu ya chama na uwajibikaji wenye tija na dhamira ya dhati ya CCM ya kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi kwa muktadha wa siasa za ushindani chini ya mfumo wa vyama vingi.
Hayo ameyasema katika mahojiano maalum ya kutoa tathmini yake ya mafanikio na uimara wa CCM katika medani za kisiasa nchini.
Sababu za Ushindi wa Kishindo
Dkt. Dimwa amebainisha kuwa ushindi wa asilimia 99 wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni matokeo ya utendaji bora wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi .
Ameeleza kuwa CCM imeshinda kwa kiwango hicho kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi wote mijini na vijijini, kuimarisha huduma za kijamii, na kutoa fursa za ajira kwa vijana wa rika tofauti na makundi mbalimbali ya wanawake.
"Ushindi huu ni matokeo ya uongozi thabiti na wa kujitolea wa viongozi wetu. Wananchi wameshuhudia mabadiliko ya kweli katika maisha yao. Ujenzi wa miundombinu, huduma za afya, elimu na kilimo ni baadhi ya sekta zinazoimarisha maisha ya watu wote bila ubaguzi wa kisiasa,kidini na kikabila. Hii inadhihirisha kuwa CCM ni chama kinachotekeleza ahadi zake na ni chama cha maendeleo," alisema Dkt. Dimwa.
Demokrasia na Mfumo wa Vyama Vingi
Katika mchango wake, Dkt. Dimwa alieleza kuwa ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni dhihirisho la nguvu ya demokrasia katika mfumo wa vyama vingi.
Alisisitiza kuwa siasa za ushindani ni muhimu katika kuleta maendeleo na kwamba CCM inaheshimu na kutambua mchango wa vyama vingine, ingawa CCM inabaki kuwa chama chenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya kivitendo kwa wananchi.
"Katika mfumo wa vyama vingi, ushindani ni muhimu, lakini ushindi wa CCM katika uchaguzi huu ni uthibitisho wa kwamba wananchi wanatambua juhudi za serikali yetu.
Demokrasia siyo tu kushiriki katika uchaguzi, bali ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafaidika na matunda ya demokrasia hiyo," alisema Dkt. Dimwa.
Mafanikio ya Falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R
Dkt. Dimwa pia alifafanua mafanikio yaliyofikiwa katika kutafsiri kwa vitendo falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya 4R imeleta matokeo chanya ya upatikanaji wa ushindi huo na kwamba mafanikio haya ni dhihirisho la jinsi serikali ya CCM inavyotoa huduma bora kwa wananchi, huku ikirudisha imani ya wananchi kwa serikali na kuimarisha umoja wa kitaifa.
" Tumeshuhudia maendeleo katika maeneo mengi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa huduma za afya na elimu, na uimarishaji wa uchumi wa Zanzibar. Kwa hiyo, ushindi huu unaonyesha kuwa falsafa ya Rais Samia ya 4R inatekelezwa kwa vitendo na inagusa maisha ya wananchi," alisema Dkt. Dimwa.
Ushindi wa Serikali za Mitaa kama Tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa 2025
Dkt. Dimwa alisisitiza kuwa ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni tathmini halisi ya matokeo yanayoweza kutarajiwa katika uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka 2025.
Alieleza kuwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo pia unatoa picha ya kuwa CCM ni Chama kiongozi katika siasa za Tanzania na kwamba wananchi wenyewe kwa ridhaa yao wameamua kukiunga mkono kukipigia kura nyingi za ndio kupitia mfumo huru wa kidemokrasia.
"Ushindi wa serikali za mitaa ni kielelezo cha mapenzi ya wananchi kwa CCM na dhamira ya chama chetu ni kuhakikisha kuwa kila mtaa, kila kijiji, kila wilaya na kila kisiwa kinapata maendeleo.
Huu ni ushindi wa wananchi na ni uthibitisho wa kwamba uchaguzi mkuu wa 2025 utakuwa na mafanikio makubwa kwa CCM," alisema Dkt. Dimwa.
Wito kwa Wananchi na Wanachama wa CCM
Dkt. Dimwa alitoa wito kwa wananchi wote, hasa wanachama wa CCM, kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la awamu ya pili ya uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litakalofanyika hivi karibuni.
Aliwakumbusha wananchi kuwa zoezi hili ni haki yao ya kikatiba na ni muhimu kwa kuimarisha demokrasia na uhuru wa kucgagua na kuchaguliwa nchini.
"Ni muhimu kwa kila mwananchi kuhakikisha kwamba jina lake linajumuishwa katika daftari la wapiga kura.
Hii ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania.Tunatoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili muhimu, ili kuimarisha ushiriki wetu katika uchaguzi mkuu wa 2025," alisisitiza Dkt. Dimwa
Pamoja na hayo Dkt.Dimwa, anaeleza kuwa CCM inaendelea kujizatiti na kuboresha huduma kwa wananchi, huku ikisisitiza kuwa uchaguzi wa 2025 utakuwa ni uthibitisho wa mafanikio ya chama na serikali katika kuleta maendeleo ya kweli kwa kila Mtanzania.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
30-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
30-05-2026