Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga (km107) iliyojengwa kwa kiwango cha lami
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga (km107) iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo imefanyika katika eneo la Matai Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.