KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis,amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwasimamia Viongozi wa Majimbo hasa Wabunge na Wawakilishi watekeleze kwa ufanisi ahadi walizotoa kwa Wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu uliopita.
Hayo ameyasema wakati akikabidhi vitendea kazi vikiwemo mitungi ya Gesi na Pikipiki kwa Viongozi wa jimbo la Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe.Profesa Makame Mbarawa Mnyaa.
Amesema CCM ipo kwa ajili ya kusimamia maslahi na haki za wananchi kwa kuhakikisha kila kiongozi aliyepewa dhamana ya kuwawakilisha Wananchi katika Vyombo vya maamuzi anatekeleza wajibu wake kwa wananchi.
Katika maelezo yake Mbeto,amefafanua kuwa CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao CCM itatoa kipaumbele kwa Viongozi wanaofanya kazi kwa ufanisi na waliokuwa karibu na Wananchi wao.
"Nakupongeza sana Prof.Mbarawa umefanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani ya CCM kwani changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili Viongozi na Watendaji wengi wa ngazi za Matawi hadi Majimbo ni ukosefu wa usafiri wa kutoka eneo moja kwenda jingine,lakini kwa busara zako leo umewapatia Pikipiki na akina mama kuwapa Gesi salama kwa ajili ya ulinzi wa miundombinu ya mazingira", alisema Mbeto.
Kupitia hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa hivyo Mbeto,aliwataka Viongozi na Wanachama kuhamasisha wananchi kujiunga na CCM kwa wingi.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 amesema tayari imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 98 kwa kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dk.Mwinyi.
Pamoja na hayo Mbeto,alimpongeza Mbunge huyo Prof.Mbarawa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta za maji safi na salama,miundombinu ya usafiri,afya,elimu na vikundi vya ujasiriamali na kwamba viongozi wengine waige mfano huo katika kuharakisha maendeleo endelevu ya majimbo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mkoani,Prof.Makame Mbarawa,Amewapongeza wanachama wa CCM kwa kazi kubwa wanayofanya ya kukitumikia Chama kwa kujitoleo.
Alisema leongo la kutoa mitungi ya Gesi ni kuunga mkono kampeni ya mazingira za kuhamasisha matumizi salama ya Gesi majumbani badala ya kuni na mkaa.
Aidha,amesema dhamira ya kutoa Pikipiki kwa Watendaji mbali mbali wa Chama ndani ya Mkoa huo ni kuwarahisishia huduma za usafiri wakati wa utekelezaji wa Majukumu yao ya kila siku.
Katika hafla hiyo Mbunge huyo wa Jimbo la Mikoani ametoa Pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi milioni 64 pamoja na mitungi ya Gesi 200 kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo hilo.
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐓𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
22-07-2026
𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
22-07-2026
🚆 𝐓𝐔𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
22-07-2026
ZIARA YA RAIS WA MISRI-TANZANIA
22-07-2026
🔰 CCM NA ACT-WAZALENDO WASAINI MARIDHIANO YA PAMOJA YA KISIASA ZANZIBAR
22-07-2026
🎉 𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐖𝐀, 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐒𝐇𝐀-𝐑𝐎𝐒𝐄 𝐌𝐈𝐆𝐈𝐑𝐎! 🔰
22-07-2026
🔰𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐁𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐋𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀
22-07-2026
🔰𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔!
22-07-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
22-07-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
22-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
22-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
22-07-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
22-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
22-07-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
22-07-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
22-07-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
22-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
22-07-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
22-07-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
22-07-2026