Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KIMEI AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI MINGI YA MAENDELEO VUNJO
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei amesema katika kipindi cha miaka takribani minne wamepokea fedha takribani shilingi bilioni 41 kwa ajili ya miradi ya maendeleo hivyo kwa niaba ya wananchi wenzake wanamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa kwao.
Dkt Kimei amesema Jimbo lake limepata zahanati mpya 12, vituo vya afya vipya viwili - Kahe na Marangu Hedikota, upanuzi wa kituo kimoja cha Kirua Vunjo, kupandishwa hadhi kwa Himo OPD kuwa kituo cha afya kamili, miradi ya maji safi ya takribani shilingi bilioni 10.2, shule mpya za msingi na sekondari tano pamoja miradi ya umeme. Utekelezaji huu umefanya siasa za Vunjo kuwa tulivu na kukiimarisha sana Chama Cha Mapinduzi.
Ametumia jukwaa hilo pia kuomba serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kujenga mazingira ya ujirani mwema na vijiji 19 vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ili kuwapa wananchi amani na utulivu katika makazi yao.
Wananchi wa Vunjo wamemzawadia Rais Samia mbuzi dume 'Ndafu' kwa utekelezaji mzuri wa ilani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt Emanuel John Nchimbi kwa uimarishaji mzuri wa Chama pamoja na sekretarieti yake.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.