Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Wazanzibari na Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuacha rushwa muhali wa kutkataa kutoa ushahidi kwa wale ambao wamepatikana na makosa ya udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto.

alternative

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid ISLAH JANG’OMBE WAYANI  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema ni lazima wazanzibari na waumini wa dini zote kushirikiana na kuwa wawazi na kuacha muhali kwa kwenda  kutoa ushahidi mahakamani au sehemu za kisheria kwa muhusika wa kosa la udhalilishaji ili kuirejeshea heshima nchi yetu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wasimamizi na watowaji wa haki katika vyombo vya sheria kuhakikisha wanatoa haki kwa kila mwananchi anaefikwa na tatizo ili waweze kuwa na imani na mihimili hio sambamba na kuwataka kutomuonea mtu yoyote katika kutoa hukumu kwa sindikizo au matwaka ya watu fulani.

Alhajj Hemed amewataka waumini na  Wazanzibari kuomba dua maalum ya kuiombea nchi ili Mwenyezi Mungu aliondoshe kabisa janga hili la udhalilishaji  janga ambalo linaiondolea sifa njema nchi yetu.

Akizunguzia suala la madawa ya kulevya  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla kutokuwafumbia macho wale waote wanaoshiriki katika kuingiza nchini dawa hizo, kutumia, kusambaza Uraibu huu ambao unaondosha nguvu kazi za vijana.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Maalim ABDUL- HAKIM ABDALLA amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuishi kwa wema na ihsani na majirani zao  ikiwa ni miongoni mwa kufanya ibada na kumcha Mwenyezi Mungu, pamoja na kuwalea watoto wao kaatika malezi yanamrizisha Allah (S.W)

Amesema kuwa suala la kuhimizana kufanya ibada lianzie kwa jirahi yako na watu tunaoishi nao katika maeneo yetu kufanya huvyo ni  kufuata nyayo za mtume Muhamad (S.A.W)  na kuongeza mapenzi baina yetu.

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi