Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS DKT. SAMIA AMEIFUNGUA KATAVI KIMAENDELEO KATIKA KILA NYANJA - MWENEZI MAKALLA
> Asema Bandari ya Karema yafungua wigo wa Uchumi na Biashara kwa Tanzania na Congo
> Asema mpango wa Serikali ya CCM ni kuunganisha bandari ya Karema na SGR
> Awataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuitisha mikutano ya kueleza mapato na matumizi ya fedha katika kuleta maendeleo kwa wananchi
"Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameitendea haki Katavi, Katavi imefunguka sana kimaendeleo, zamani ilikuwa ukitwa kwenye kikao Dodoma ujue ukitoka saa 12 asubuhi hapa Katavi utafika saa 12 jioni, nitoe ushuhuda mimi nilikuwa natembea na mito kwenye gari na nakaa siti ya nyuma ili nilale sababu unachoka lakini kwa mama yetu Rais Dkt. Samia ni lami unganishi kuanzia hapa hadi kila sehemu ya wilaya na mikoa jirani."
"Katavi ilikuwa kama mkoa ambao umefungwa na ilikuwa ukiletwa huku ni kama unaletwa kushikishwa adabu lakini kwasasa hata huduma za usafiri wa Anga zinapatikana hapa Katavi na hii imepeleka kutanua na wigo wa utalii."
"Nakumbuka nilitoka hapo kukiwa na wazo la kujengwa bandari karema (upande wa tanzania na pacha wake ni kule Nchini Congo) kwasasa bandari imejengwa na uchumi na biashara kati ya Congo na Tanzania utahimarika maradufu na bandari hii itaunganishwa na SGR (reli ya kisasa) yote haya ni maendeleo."
"Ujenzi wa hospitali ya mkoa chini ya SUMA JKT Awamu ya kwanza imekamilika, tumefurahi kusikia hivyo hakika Wanachama wote pokeeni mafanikio haya na muwe sehemu ya kuyasemea."
"Mkoa wa Katavi haujaunganishwa na gridi ya taifa kwenye Umeme lakini niwape siri tuu, kero hiyo itaisha kwakuwa serikali ya CCM itaunganisha kupitia mkoa wa Tabora ilikusudi viwanda vyetu kufanya kazi kwa ufasaha."
"Niwatake Wenyeviti wa Serikali za Mitaa itisheni mikutano ya wananchi kueleza taarifa za mapato na utekelezaji wake kwa kuleta maendeleo."
Ndugu. Amos Makalla
Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa
Ameyasema hayo kwenye Mkutano wa kueleza muelekeo wa Chama pamoja na mambo mengine kuhusu uelekeo wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mkutano huu umekutanisha, Wajumbe wa Mashina na Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji na Miitaa, Viongozi wa Chama ngazi zote, Wazee mashuhuri, Viongozi wa Dini pamoja na Watendaji wa serikali ngazi zote na Taasisi zisizo za kiserikali.
🗓️ 13 Aprili, 2024
📍Mpanda - Katavi
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.