Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


ANAYETAFUTA MADARAKA KWA MAFARAKANO HAFAI NDANI YA CCM - BALOZI DKT. NCHIMBI

alternative

"Mtu yeyote anayetafuta madaraka kwa mafarakano, kwa misingi ya ukabila, kwa misingi ya dini hawafai kuwa kiongozi wa serikali wala katika chama chetu cha mapinduzi, kila mtanzania anatakiwa kukumbuka kuwa viongozi sahihi wataisimamia serikali sahii"

"Chama kibovu kitazaa serikali mbovu, chama kisicho makini kitazaa serikali isiyo makini, chama imara kinaanza kujengwa katika mashina, tutambue kwamba hiyo ndio ngazi ya kwanza ya umuhimu wa pekee katika chama chetu na wao watambue wao ndio wa kwanza kuusimamia wajibu wa wananchama"

"Hii ndicho chama pekee kinachoongelea majukumu ya chama kwa wanachama wake na huwezi kuyatenganisha mafanikio ya serikali na CCM kwakuwa CCM madhubuti ndio yenye kuleta maendeleo kwa taifa hili."

Sambamba na hayo Katibu Mkuu amekumbusha nafasi ya mwanachama wa CCM, "Tunawakumbusha viongozi wetu kuwa CCM ni mali ya wanachama si mali ya mtu binafsi...maana unakuta kuna kiongozi mwingine haoni tabu kumwambia mwanachama wa kawaida kuwa mimi ndio mwenyekiti wa tawi nimefika hapa na hunifanyi lolote na nenda popote...ndani ya CCM hilo halikubaliki"

"Hakuna atakayeweza kuwa kiongozi wa CCM bila kuwa mwanachama, nafasi pekee ambayo mtu anaapishwa kwenye CCM ni Uanachama, hakina sehemu nyingine zaidi ya hapo ndio maana hamjawahi kusikia hata mwenyekiti wa CCM Taifa akiapishwa ndani ya Chama"

Hayo yamesmwa na Balozi Dkt. Nchimbi.

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amewataka wana CCM kuwa na utaratibu wa kujikumbusha majukumu ya unachama wa kwa kusoma katiba ya CCM.

" Ibara ya 15 kifungu cha kwanza kinaeleza wajibu wa kila mwanachama, tuwe na utaratibu wa kujikumbusha kwa kusoma katiba ya chama chetu cha mapinduzi ." 

 WAJIBU MKUBWA WA CCM NI KUJENGA UMOJA  Kauli ya Katibu Mkuu wa CCM.

"Hatutajenga CCM ikawa imara kama hatutakuwa na umoja miongoni mwetu, CCM ikikosa umoja itasambaratika na Nchi itasambaratika , Baba wa Taifa alisema na napenda kurudia hili ' Mimi nang'atuka lakini naendelea kuamini kuwa bila CCM madhubutu Nchi hii itayumba ' maneno haya yanaishi hadi leo.

"Wakati mwingine linaweza likatokea jambo dogo likatutawanisha, tujiepushe na mambo ya kututenganisha tusiruhusu kabisa mafarakano kati yetu"

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM

🗓️16 Aprili, 2024
📍Mbozi - Songwe

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi