Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) na wanachama wake kuyatumia vyema mafunzo wanayopatiwa ambayo yatawajengea uwezo wa utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika Chama cha Mapinduzi sambamba na kutatua changamoto za wanachama zinapojitokeza
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa Semina ya siku moja ya kuwaongezea ujuzi na maarifa Madiwani, Makatibu wa Wadi na Majimbo pamoja wajumbe wa kamati tendaji iliyofanyika katika ukumbi wa Viwanja vya Maonesho Nyamanzi Zanzibar Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Mhe. Hemed ameseama moja ya jukumu la UWT ni kutoa elimu kwa wanachama, kuwahamasisha wanawake katika kugombea nafasi za Uongozi, kuishauri Serikali na kutatua changamoto katika jamii kwa lengo la kuweka mustakbali mwema wa Taifa na chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushika Dola awamu kwa awamu.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Uongozi ni kuonesha njia kwa wanowaongoza ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kusema kuwa kufuata maadili ya Uongozi na Utendaji ni jambo la msingi ambalo litasaidia kunyanyua ari kwa wafuasi wa Chama na kuleta maendeleo kwa Jumuiya.
Aidha Mhe. Hemed ametoa wito kwa Viongozi kuzitumia vyema nafasi zao kwa kufuata misingi ya uongozi kwa wanowaongoza ikiwemo nidhamu, uaminifu, uadilifu, unyenyekevu, kujenga umoja, matumizi mazuri ya lugha, kutatua kero na kuandaa viongozi wapya watakaoweza kushika nafasi mbali mbali katika Jumuia.
Sambamba na hayo, Mhe Hemed amesema anatambua kuwa wapo baadhi ya viongozi na watendaji hawana lugha nzuri kwa wanowaongoza hivyo amewataka kujirekebisha na kuachana na tabia hiyo kwani Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia mtu yoyote atakae kwenda kinyume na maadili ya Chama, hivyo amewahamasisha wanawake ndani ya Chama Cha Mapinduzi wenye uwezo wa kuongoza kujiandaa na kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika Uchagzi Mkuu wa mwaka 2025.
Kwa upende wake Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Mary Pius Chatanda amezipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukamilisha vyema na kwa mafanikio makubwa zoezi la sensa la kidigital ambalo halijawahi kutokea nchini ambalo takwimu zake zitalisaidia Taifa katika kupanga mikakati mbali mbali ya kimaendeleo nchini.
Chatanda amewaagiza viongozi ambao wamepatiwa mafunzo hayo kushuka kwa wananchi kusikiliza kero zao zinazowakabili ili kuweza kufanya maamuzi sahihi katika vikao vya chama na Serikali.
Aidha amewataka viongozi wa UWT kuendelea kufanya zoezi la usajili wa wanachama wapya kwa njia ya kielektroniki ambao watasaidia katika kupanga mikakati ya Jumuiya sambamba na kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Mapema Makamo Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Zainab Khamis Shomari amesema kuwa Mafunzo hayo waliopatiwa viongozi wa UWT yataleta mabadiliko chanya katika Utendaji kazi wa Jumuiya na Chama kwa Ujumla.
Amesema kuwa UWT wamejipanga kukipigania na kukilinda chama cha Mapinduzi kwa kuhakikisha kinafanya vizuri katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka huu na ule uchaguzi Mkuu wa nchi mwaka 2025 CCM inashinda na kuendelea kuiongoza nchi.
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
31-05-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
31-05-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
31-05-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
31-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
31-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
31-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
31-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
31-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
31-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
31-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
31-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
31-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
31-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
31-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
31-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
31-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
31-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
31-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
31-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
31-05-2026