Serikali imeanza Uchunguzi Maalumu wa kubaini mapungufu mbalimbali katika Viwanja vyote vya Ndege nchini
" Ili kubaini changamoto hilizopo na kuweza kuzifanyia kazi ikiwemo Mapungufu ya Kimfumo,Utendaji na Upungufu wa Miundombinu ili kuweza kuboresha sehemu husika lengo ikiwa kurahisisha uingiaji na utokaji wa wageni ikiwemo watalii wanoukuja nchini kwa shughuli za utalii ambao uiingizia nchi kiasi kikubwa cha fedha sambamba na kudhibiti uhalifu unaotokea katika Viwanja vya Ndege ikiwemo utoroshaji wa vito vya thamani,mnyororo wa upitishaji na uingiaji wa dawa za kulevya na uingiaji nchini kwa wageni bila kufuata sheria na taratibu za kiuhamiaji ".
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama ambapo kamati hiyo ilitembelea na Kukagua Mifumo ya Uhamiaji Mtandao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Ujenzi wa Chuo cha Uhamiaji Kitogani na Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Mjini Magharibi Mazizini.
‘Mbali ya kazi nzuri ambazo zinafanywa na Uhamiaji lakini kuna maeneo tunataka kupeleka nguvu zaidi hasa maeneo ambayo kwanza ni sura ya nchi,malango makuu ya kuingilia kama hapa tulipo katika maeneo ya Viwanja vya Ndege,mtu akija Tanzania sura ya nchi inamuonyesha anapopokelewa katika viwanja vya ndege,haipendezi mgeni akija hapa nchini apange mstari mrefu,mara viyoyozi havifanyi kazi ndio maana serikali kuna uchunguzi maalumu tunafanya ili kuweza kubaini mapungufu hayo na kuyafanyia kazi katika Viwanja vyote vya ndege nchini.’ Alisema Waziri Masauni
Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vicent Mbogo amesema ni muhimu mapungufu hayo katika viwanja vya ndege yakafanyiwa kazi huku akisifu juhudi za serikali zote mbili katika kuiletea Zanzibar maendeleo ambapo alisema Zanzibar ni nchi ya utalii ni vyema huduma malango yan chi zikaboreshwa.
‘Zanzibar imeendelea kwa kasi kubwa pamoja na maendeleo haya ya miundombinu katika uwanja wa ndege ambapo sasa yanasomana na kule Tanzania Bara tumeona maendeleo yanafanyika katika viwanja vyetu ambavyo ndio maingilio ya watalii ambao wanatuletea fedha nyingi hapa nchini,napenda kwapongeza Marais wetu,Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ali Mwinyi wanafanya kazi kubwa sana kuiletea nchi yetu maendeleo’alisema Mbogo
Nae Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan alitaja jinsi miradi ya maendeleo ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 ilivyokamilika ikiwemo Ujenzi wa Ofisi ya Uhmiaji mkoa wa Mjini Magharibi,Mkoa wa Kusini Pemba,Ukarabati wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar,Ukarabati wa Nyumba ya Makazi ya Askari Ndugu Kitu Chake Chake Pemba na Ukarabati wa Nyumba Mbili za Makaazi ya Askari Mtemani Wete na Pemba ambapo imekamilika kwa asilimia mia moja huku gharama yake ikiwa ni kiasi cha Shilingi Bilioni1.9 .
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
04-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
04-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
04-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
04-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
04-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
04-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆’-𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀
04-06-2026
𝐍𝐈 𝐍𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀!
04-06-2026
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
04-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
04-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
04-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
04-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
04-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
04-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
04-06-2026