Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


ππ€π‹πŽπ™πˆ πƒπŠπ“. ππ‚π‡πˆπŒππˆ π€π–π€ππŽππ†π„π™π€ π–π€π‡π€π‘πˆπ‘πˆ 𝐖𝐀 π•π˜πŽπŒππŽ π•π˜π€ π‡π€ππ€π‘πˆ πŠπ–π€ πŠπ”πƒπ”πŒπˆπ’π‡π€ 𝐍𝐀 πŠπ”π„ππƒπ„π‹π„π™π€ π€πŒπ€ππˆ π˜π€ ππ‚π‡πˆ π˜π„π“π”

alternative

πŸŽ₯Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewapongeza wahariri wa vyombo vya habari kwa kutumia taaluma yao vizuri katika kulinda, kudumisha na kuendeleza amani iliyopo nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano maalum wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) , Dkt. Nchimbi amesema ukomavu wao katika kuchuja na kufuata sheria na haki wakati wa uandishi umeifanya nchi kutokuwa kwenye majuto.

"Wahariri wa vyombo vya habari ambao ninyi ndio mnaruhusu habari yoyote itoke kwenye chombo cha habari kama mngetumia nafasi yenu vibaya kwa miaka yote mliyofanya kazi yenu inawezekana nchi yetu isingekuwa hivi leo"

"Wahariri wa vyombo vya habari kwa mfano wakiamua kutengeneza msongo wa mawazo kwa raia wanatengeneza...mkiamua kulikuza jambo mnaweza na mkiamua kuchochea jambo mnaweza, wahariri ndio chujio la habari zote katika Taifa"

"...kwa kweli mimi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi na kwa niaba ya Watanzania wapenda Amani, nawashukuru sana Wahariri kwa kupitia Waandishi wa habari"

#KaziNaUtuTunasongaMbele

alternative alternative
Habari Nyingine