Makabidhiano - Dar Es Salaam
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wana-CCM na wananchi kwa ujumla waendelee kuiamini Serikali yao kwa sababu watendaji wake wamejipanga kuwatumikia kwa weledi, uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.
Pia, Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM Taifa amefanya maboresho makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uwekezaji lengo likiwa ni kukuza uchumi wa Taifa na wa mwananchi mmoja mmoja.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 5, 2023) wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 46 ya CCM Mkoa wa Kagera. Maadhimisho hayo kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa CCM wilayani Biharamulo.

Amesema Serikali imeboresha mazingira ya uwekezaji na kuvutia uwekezaji kwenye sekta za madini, kilimo na viwanda ikiwa miongoni mwa mikakati ya Serikali ya kupambana na changamoto ya ajira hususan kwa vijana.

"Mheshimiwa Rais Dkt Samia amejikita katika kutatua changamoto ya ajira nchini kwa kupanua wigo wa uwekezaji na kuwakaribisha waje wawekeze nchini wajenge viwanda. Uwekezaji katika kilimo, viwanda ndio jibu la tatizo la ajira."

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza watendaji wa halmashauri wahakikishe vijana wanapatiwa maeneo ya kilimo na hati pamoja na kuwapa kipaumbele katika utoaji wa mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato yao ya ndani.

Akizungumzia kuhusu maslahi ya wtumishi wa umma, Waziri Mkuu amesema CCM imeielekeza Serikali isimamie ipasavyo maslahi yao ikiwa ni pamoja na kulipa madeni na malimbikizo mbalimbali pamoja na upandishwaji wa madaraja, hivyo amewataka waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watanzania kwa kuiunga mkono CCM katika utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi ya 2020 ambayo imeainisha mambo mbalimbali ya maendeleo yanayotekelezwa nchi nzima ukiwemo na mkoa wa Kagera.

DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
18-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
18-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
18-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
18-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
18-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
18-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
18-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
18-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
18-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
18-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
18-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
18-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
18-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
18-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
18-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
18-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
18-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
18-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
18-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
18-11-2025