Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
WANASIASA TUCHUNGE NDIMI ZETU-NCHIMBI
WANASIASA TUCHUNGE NDIMI ZETU-NCHIMBI
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewataka wanasiasa nchini, kutumia vizuri ndimi zao na kamwe wasitoe matamshi ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.
Balozi Dk. Nchimbi ameyasema hayo Jumanne Agosti 13, 2024 alipokua akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja, Geita Mjini.
Balozi Nchimbi amesema wanasiasa wasijisahau katika kuchagua maneno yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi yetu, na kuongeza kuwa wako watu ndani ya wanajisahau, hivyo amewaomba Watanzania wasijisahau.
“Wana CCM na Wanasiasa wa vyama vingine wachague maneno wanayoyatumia, kwani wote wanajenga Nchi moja inayoitwa Tanzania ambayo wana wajibu wa kuipenda na kuitumikia kwa nguvu zote.”,amesema Nchimbi
Dkt. Nchimbi anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuimarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi.
Katika ziara hiyo Balozi Dkt.Nchimbi ameambatana na Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.