Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS SAMIA ASHEREHEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA NA WAJUKUU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Ndg. Samia Suluhu Hassan akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.
Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema, na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.