Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Serikali imeanza Ufungaji wa Kamera maalumu(CCTV) katika maeneo mbalimbali yanayozunguka magereza lengo ikiwa ni Uboreshaji wa Huduma za ulinzi na usalama pamoja na kwenda na dhana nzima ya sayansi na teknolojia katika utoaji na ufuatiliaji wa huduma kwa wadau mbalimbali wanaoshilikiana na Jeshi la Magereza ikiwemo Jeshi la Polisi na Mahakama.
‘Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha jeshi katika maeneo mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake, baadhi ya maeneo hayo ni ununuzi wa vifaa vya ulinzi na usalama katika maeneo yanayozunguka magereza kwa nje ambapo kwa sasa zoezi la usimikaji wa vifaa hivyo kwa sasa unaendelea katika maeneo ya magereza ya Maweni, Karanga, Moshi, Lwanda na Tabora’.alisema
Ameyataja maeneo mengine yaliyoboreshwa na serikali ya awamu ya sita kuwa ni vyombo vya usafiri,ajira,upandishwaji vyeo kwa askari na maafisa ambapo hadi sasa jumla ya ajira 662 ziko katika mchakato wa usaili huku upandishwaji vyeo mpaka sasa askari na maafisa 4111 wamepandishwa vyeo.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo amewataka Askari wa Jeshi la Magereza kuwa ni nidhamu katika utendaji wao wa kazi ili kujiepusha na tuhuma mbalimbali ambazo zitalichafua jeshi huku akimpongeza Rais Daktari Samia Suluhu Hassani kwa msaada anaotoa kwa vyombo vya ulinzi na Usalama likiwemo Jeshi la Magereza.
‘Sifa kubwa ya askari ni nidhamu,nidhamu hiyo inapaswa kuanzia ndani ya jeshi mpaka nje,nawaomba muendelee kuboresha nidhamu kazini ili kuboresha mahusiano yenu pamoja na viongozi wenu jueni mheshimiwa Rais anawategemea sana katika utoaji wa huduma na maelekezo yake ni kuwa Tume ya Haki Jinai ilishatoa mapendekezo sasa yafanyiwe kazi ili kuondoa baadhi ya changamoto ikiwemo msongamano wa wafungwa magerezani’ alisema Naibu Waziri
Naibu Waziri Daniel Sillo ameaza ziara rasmi katika vyombo vya ulinzi vilivyopo ndani ya wizara baada ya muda mfupi kuteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhudumu katika nafasi hiyo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.