GAVU AHIMIZA WANACHAMA KUENDELEA KUHAMASISHA WATANZANIA KUIPA DHAMANA CCM
Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndugu. Issa Haji Gavu ameendelea kuwahimiza wanachama wa CCM kujua na kutambua kwamba ushindi kwa CCM ni jambo la umuhimu na lazima kwakuwa chama chochote cha siasa kinahitaji kura ili kushika dola hivyo amewaomba kuendelea kuhamasisha watanzania wote kuendelea kukipa dhamana Chama Cha Mapinduzi na hamasa hiyo iendane kwa kuyasema makubwa yaliyofanywa na serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndugu. Gavu ameyasema hayo wakati akizungumza na Mabalozi wa mashina, viongozi wengine mbalimbali wa CCM, Viongozi wa Serikali, Wazee, Viongozi wa dini na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali Mkoani Ruvuma.
ποΈ20 Aprili, 2024
πSongea Mjini - Ruvuma