Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Wazazi na walezi wametakiwa kuwasimamia watoto wao katika suala zima la kufanya Ibada hasa katika mwezi wa Ramadhan ambao ni mwezi wenye fadhila nyingi ambao humtakasa mja kutokana na maovu na machafu.

alternative

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid SHEYKHAT  NAIMA uliopo TOMONDO MADUKA saba(7)  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema kuwa kuwasimamia vyema vijana katika kufanya Ibada na kuwapa elimu juu ya kuijua dini yao pamoja  na nchi yao kutapelekea Taifa kupata viongozi bora na wenye kufanya kazi kwa maslahi ya nchi  na Taifa kwa ujumla.

Alhajj Hemed amesisitiza kuwa zimebaki siku chache kuingia kwa  mwezi mtukufu wa ramadhani hivyo ni vyema waislamu kuongeza bidii katika kuwahimiza vinjana wao kufanya ibada ikiwemo visimamo vya usiku, kuhudhuria madrasa na kupendana baina yao ambako kutapelekea kupata wanazuoni walio bora na wenye kuijua dini yao.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema katika mwezi wa Ramadhani waumini wanapaswa kuzidisha upendo na mshikamano baina yao sambamba na kutoa sadaka kwa kuwasaidia watu wasio na uwezo  ili kupata fadhila za mwezi mtukufu wa ramadhani.

Sambamba na hayo  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar  kuendelea kudumisha mila, silka na desturi zilizopo nchini hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhania kwa  kuacha kuvaa nguo zisizofaa ambazo zitawapelekea waumini wa dini ya kiisalumu kutokufikia lego la kufunga.

Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh. KASSIM HAMAD amewaasa waumini wa Dini ya Kiislam kuacha tabia ya kuingila  Mamlaka ya Taasisi za Kiserikali hasa Taasisi iliyopewa dhamana ya kutangaza kuandama kwa mwezi hususan Mwezi mtukuru wa ramadhan kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za nchi na za dini ya Kiislamu.

Amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya  waislamu kufarakana na kutosaidiana kutokana na tofauti zao za kimadhehebi  katika kufuata muandamo wa mwezi hivyo amewasisitiza waislamu kujiepusha kabisa na matendo hayo kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maamrisho ya  Allah (S.W) na kutapelekea kutokufikia lengo la kufunga.

 

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi