Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Samia kupitia Nchimbi akamilisha ahadi Manyoni
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan leo kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amekipatia chama wilaya ya Manyoni zaidi ya shilingi millioni 18 kwa ajili ya kuezeka jengo lake la kitega uchumi.
Katibu Mkuu wa CCM alitangaza hayo mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, mjini Manyoni, mwanzoni mwa ziara yake ya siku mbili mkoani Singida.
Amesema hiyo ilikuwa ni ahadi ya Mwenyekiti Rais Samia aliyoitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa zamani Daniel Chongolo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.