Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, imeweka Sera na Mikakati mbali mbali pamoja na kuchukua hatua za kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kukamilisha malengo yao na kuweza kutoa mchango katika kuliendesha Taifa.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kufunga Maadhimisho ya Miaka kumi na Tano (15)ya Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip uwanja wa ndege Zanzibar.
Mhe. Rais Dkt Samia amesema kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na watu wenye Ulemavu Serikali imeweza kutoa nafasi za uongozi kwa watu wenye ulemavu katika Wizara mbali mbali nchini ambapo wanaendelea kufanya vizuri katika majuku yao siku hadi siku.
Amesema kuwa Serikali imeanzisha Mabaraza ya Watu wenye Ulemavu kwa wilaya zote za Unguja na Pemba ambayo yanasaidi upatikanaji wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu katika Taasisi zote za Umma na kuleta haki na fursa za watu wenye ulemavu nchini.
Aidha Serikali imeanzisha Mfumo wa Maendeleo ya watu wenye Ulemavu ambao katika mwaka wa fedha 2023-2024, Serikali imetenga Bajeti ya Shilingi milioni mia mbili(200, 000,000) kwa lengo la kuwanufaisha watu wenye Ulemavu kujiendeleza Kiuchumi.
Sambamba na hayo Rais Dkt Samia amesema Serikali inaendelea kutoa Mikopo kwa wajasiriamali na kwa kuweka kipaumbele kwa watu wenye Ulemavu kupitia fedha za ahueni ya UVIKO 19, fedha za mapato yatokanayo na Serikali pamoja na Mfuko wa Khalifa Foundation Fund kupitia wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar.
Amefahamisha kuwa Serikali imejenga Skuli mbili (2) za Dahalia kwa watu wenye Ulemavu Unguja na Pemba kwa lengo la kuhakikisha watu wenye Uemavu wanaendelea kupata fursa sawa za elimu kama watu wengine sambamba na kutunga Sheria ya watu wenye Ulemavu Nam.(8) ya mwaka 2022 kwa lengo la kuwalinda na kutetea haki na fursa za watu wenye Ulemavu wakiwemo wanawake.
Dkt Samia amesema Serikali imekuwa ikiwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika mashindano ya Kimataifa yaliyofanyika katika nchi mbali mbali Duniani sambamba na kushiriki katika Warsha iliyoshirikisha Mataifa Kumi na Tano(15) yenye lengo la kutoa Mafunzo na kutayarisha wataalamu wa Michezo Jumuishi itakayowajumuisha watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu bila ya kuwa na Utengano wa aina yoyote.
Rais Dkt Samia ametoa wito kwa Taasisi za Serikali, Sekta binafsi na washirika wa Maendeleo kuiunga mkono JUWAUZA na Taasisi nyengine za watu wenye Ulemavu pamoja na kuitaka jamii kuendelea kutoa mashirikiano kwa watu wenye Ulemavu ili waweze kushiriki katika Ujenzi wa Taifa.
Mapema kaimu waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratib na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma amesema JUWAUZA ni Taasisi ya kupigiwa mfano na kuigwa kwa namna wanavyoisaidia Serikali katika kupambania haki za wanawake na wasichanya wenye ulemavu Zanzibar kwa kuona kuwa wanathaminiwa na kupewa kipaumbele katika shuhli mbali mbali za Kimaendeleo.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuthamini michango inaotolewa na Jumuiya ya JUWAUZA na kuahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendela kushirikiana nao katika kufikia adhma na malengo ya jumuiya hio yanafikiwa.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar Ndugu Abdulwakil Haji Hafidh amesema JUWAUZA Inasimamia haki za wanawake na wasichana wenye Ulemavu kwa kuwapatia elimu, ushirikishwaji katika mambo mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na Kisiasa.
Amezishukuru serikali zote mbili kwa kuwaamini na kuwathamini wanawake kutoka jumuiya ya wanawake wenye ulemavu JUWAUZA kwa kuwapa nafasi mbali mbali za uongozi katika serikali pamoja na mihimili ya kutunga sheria nchini, na kufanya vizuri siku hadi siku katika kulilitea taima maendeleo.
Mwakilishi Mkaazi kutoka UN Bwana ZLATAN MILISIC amesema watu wenye uemavu hasa wanawake na watoto wanastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa kwa kupatiwa haki zote stahiki sawa na wengine ili waweze kufanikisha malengo yao waliojiwekea.
Pia ameziomba serikali zote mbili kushirikiana na JUWAUZA kuhakikisha watu wenye Ulemavu hasa wanawake na wasichana wanapatiwa Elimu, Ujuzi, Nyenzo na maarifa kwa kuweza kufanya kazi katika Taasisi Mabali mabali, kushirikishwa katinga ngazi za maamuzi na katika kutunga Sera na Mipango ya Maendeleo ya Nchi.
Amesema wakati umefika wa Jamii, wazazi na walezi kuwakubali na kuwapa mashirikiano watu wenye Ulemavu, kuwashajihisha kwa kuwashirikisha katika shuhuli mbali mbali zinazofanyika katika jamii ili na wao wajione wana mchango katika jamii na Taifa sawa na wengine.
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐓𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
26-07-2026
𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
26-07-2026
🚆 𝐓𝐔𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
26-07-2026
ZIARA YA RAIS WA MISRI-TANZANIA
26-07-2026
🔰 CCM NA ACT-WAZALENDO WASAINI MARIDHIANO YA PAMOJA YA KISIASA ZANZIBAR
26-07-2026
🎉 𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐖𝐀, 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐒𝐇𝐀-𝐑𝐎𝐒𝐄 𝐌𝐈𝐆𝐈𝐑𝐎! 🔰
26-07-2026
🔰𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐁𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐋𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀
26-07-2026
🔰𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔!
26-07-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
26-07-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
26-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
26-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
26-07-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
26-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
26-07-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
26-07-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
26-07-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
26-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
26-07-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
26-07-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
26-07-2026