KATIBU MKUU WA CCM AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MKAAZI WA SHIRIKA LA FES UJERUMANI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Friedrich Ebert Stiftung (FES) la nchini Ujerumani, Bwana Christian Denzin, aliyefika ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumza mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya CCM na FES, leo tarehe 19 Septemba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar ES Salaam.