Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Chama cha Mapinduzi kiko imara na kitaendelea kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Jimbo la Kwahani na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020-2025 kutokana na kuitekeleza vyema Ilani ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Akimnadi Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kwahani kupitia tiketi ya CCM Ndg Khamis Yussuf Mussa Pele wakati wa kufunga kampeni za jimbo hilo katika viwanja vya kibanda maiti , Mhe. Hemed amewataka wananchi wa Jimbo la kwahani kumpigia kura za ndio mgombea huyo ili aendeleze kuinadi na kitekeleza vyema ilani ya CCM.
Amesema endapo wananchi wa jimbo la Kwahani hawatafanya makosa na watamchagua ndugu Pele kuwa mbunge wa jimbo hilo ambae atashirikiana na wabunge na viongozi wengine katika kuitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hasa katika kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo.
Mhe. Hemed amewataka wana CCM wa jimbo la kwahani kudumisha amani na utulivu wakati wote wa zoezi la uchaguzi na kuwasihi watakapomaliza kupiga kura kuŕudi majumbani kusubiri matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib amesema wana CCM wa jimbo la kwahani wanaahidi kumchagua kwa kishindo ndugu Khamis Pele ambae anatosha kuwa Mbunge kutokana na uchapa kazi wake katika chama, uaminifu na kujitoa kwake katika kuitumikia CCM vinatosha kuipeperusha bendera ya CCM katika Bunge.
Talib ametoa onyo kali kwa wale wote wanaotumia majukwaa kwa kuwatukana na kuwakashifu Viongozi wakuu wa nchii na kusema kuwa CCM haitakuwa tayari kuvumilia uovu huo na itaviomba vyombo vya sheria kufanya kazi yake kwa maslahi ya Taifa.
Akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani ndugu Kahamis Yussuf Pele ameahidi ataitekeleza vyema Ilani ya CCM kwa kukaa pamoja na viongozi wengine wa Jimbo kupanga mikakati ya kimaendeleo ili kuweza kuleta Ustawi ndani ya Jimbo hilo la kwahani.
Pele amewashukuru Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa imani kubwa waliyompa ya kumteuwa kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kwahani ambapo amesema kazi yake kubwa ni kuhakikisha anayatekeleza kwa vitendo yale yote yaliyoelezwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
27-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
27-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
27-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
27-06-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
27-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
27-06-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
27-06-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
27-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
27-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
27-06-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
27-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀!!
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐊𝐔𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎
27-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐀𝐕𝐔𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐄𝐌𝐁𝐄, 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈
27-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀𝐀, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐀𝐍𝐙𝐈𝐀 𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈!
27-06-2026
𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟏𝟎% 𝐘𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐋𝐔𝐌
27-06-2026
𝐍𝐃𝐆 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐑𝐔𝐕𝐔𝐌𝐀, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐃𝐈𝐎 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌
27-06-2026
𝐊𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐀𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
27-06-2026
𝐌𝐇𝐄. 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐍𝐀𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀, 𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐈𝐙𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐄𝐍𝐔 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐅𝐔: 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀
27-06-2026