KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM YA TAIFA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 1 Oktoba, 2023, ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichofanyika jijini Dar Es Salaam.