Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MACHA ASHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA ASASI YA KIRAIA YA WANAWAKE VIJANA WA AFRIKA - YOUNG WOMEN OF AFRICA (YWOA)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Anamringi Macha akizungumza wakati wa kutoa salaam za CCM, Jumanne, Disemba 12, 2023, kwa viongozi vijana wanawake kutoka nchi 16 za Afrika wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Asasi ya Kiraia ya Young Women of Africa (YWOA), wanaotoka katika vyama tawala katika nchi hizo. Mkutano huo unaoendelea katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, iliyoko Kibaha, mkoani Pwani, unafanyika sambamba na mafunzo na mijadala ya masuala anuai yanayowahusu wanawake na uongozi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii za Afrika na dunia kwa ujumla na kuweka maazimio yatayakochangia mstakabali wa jamii zilizo bora zaidi kwa kila mmoja.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.