Mhe Hemed Suleiman amewataka wahudumu wa afya kuwa na bidii na nidhamu kwa wananchi
Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Madinat - Albahr Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akifungua mkutano wa 14 wa Mapitio na Mpango wa pamoja wa Utekelezaji katika Sekta ya Afya.
Amesema kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ni kufuata msingi wa maadili ya kazi ya utoaji wa huduma za afya kutasaidia kupunguza malalamiko yanayotolewa na baadhi ya hudumu wakati wa kuwahudumia wagonjwa.
Mhe. Hemed amewaomba Washirika wa Maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kuisaidia Wizara ya Afya kwa kuweka miundombinu ya kidijitali ya ukusanyaji wa taarifa za afya ili juhudi zinazochukuliwa na Serikali na Wadau ziweze kutatua changammoto ikiwemo ya upatikanaji wa taarifa sahihi za takwimu za afya.
Nae Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa bila ya kuimarisha afya ya msingi hawatafikia malengo hivyo wataendelea kuimarisha miundombinu na vifaa tiba vya kisasa ili kutoa huduma bora kwa jamii.
Waziri Mazrui ameeleza kuwa vifo vya watoto vimepungua kutoka 1940 kwa mwaka 2023 hadi kufikia 1847 kwani lengo la Serikali ni kupunguza vifo vya mama na mtoto
Aidha amewasisitiza madaktari na wataalamu wa Afya kubuni miundombinu bora itakayoweza kuwasaidia mama wajawazito ili kupunguza kifafa cha mimba sambamba na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt Amuor Suleiman amesema kuwa kwa mwaka 2022 hadi 2024 Wizara imefanikiwa kutoa huduma za afya katika vituo vya ngazi ya chini (vituo vidogo) pamoja na kuanzisha mfuko wa huduma za afya kwa ajili ya kutoa huduma bora nchini ambapo Serikali imetenga bilioni 344 kwa Sekta ya Afya ili kuimarisha afya za wananchi.
Aidha amefahamisha kuwa Wizara imefanikiwa kuzalisha hewa tiba pamoja na kununua Magari makubwa ambayo yanatoa huduma za afya, ambulance kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, kununua vifaa vya kugundukia maradhi yanayowakabili wananchi ikiwemo kansa Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika.
Akizungumzia maradhi yanayoongoza hadi kufikia sasa ni pamoja na maradhi ya mfumo wa hewa, maradhi ya kuharisha pamoja maradhi ya UTI, ipo haja ya kutilia mkazo kwa mwaka ujao ili kupunguza matatizo hayo.
Dk Amour ameeleza kuwa kwa upande wa watoto chini ya miaka mitano matatizo ya mfumo wa kupumua pamoja na maradhi ya ngozi ambapo maradhi yanayoongoza kusababisha vifo ni maradhi yasiyoambukiza hivyo mikakati madhubuti inahitajika ili kupunguza idadi ya vifo hivyo ikifuatiwa na vifo vya watoto wachhanga.
Mkutano huo umewashirikisha wadau mbalimbali wa Afya wakiwemo washirika wa kimataifa ambapo Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Uwepo wa Mfumo Bora wa Huduma za Afya ya msingi uliyoungwanishwa,ubunifu unaojengwa kwa ushahidi ili kufikia Upatikanaji wa Afya Jumuishi kwa wote”.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025