Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
HAPI AHIMIZA KAMPENI ZENYE STAHA ILI KUWAPATA VIONGOZI BORA.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Ndugu. Ally Hapi (MNEC) amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine kufanya kampeni za kistaarabu na kiungwana ili kuendelea kulinda amani na mshikamano uliopo nchini huku akihamasisha wagombea kujikita katika kueleza sera zao badala ya kutumia majukwaa kueneza siasa za chuki.
Hapi, amehutubia mamia ya wananchi na wanaccm wa Bukoba katika Uwanja wa Kashai, akihamasisha umuhimu wa kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Katika hotuba yake, Hapi alisisitiza kuwa viongozi wa CCM wamekuwa na rekodi bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, na maji chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.