NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa amesema Chama hicho kitaendelea kuwa mtetezi na mwangalizi wa Wananchi wote.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kada wa CCM ambaye ni Mkurugenzi mstaafu idara ya umwagiliaji Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt.Ramadhan Aseid Ramadhan huko nyumbani kwake Fuoni.
Dkt.Dimwa,amesema lengo la ziara yake hiyo ni kumtembelea ili kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara zake za kuwatembelea makada,wazee na wananchi kwa ujumla.
Alieleza kuwa ziara hizo zinaendeleza utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi wa kuweka daraja huru la mahusiano mema baina ya Chama na Wananchi bila kujali tofauti za kidini,kisiasa na kikabila.
"Kila nikikutana na wazee na makada wakongwe waliotumia nguvu na muda wao kuitumikia nchi yetu kwa uadilifu nafurahi sana kwani napata ushauri,mbinu na nasaha nzuri za kunisaidia katika masuala ya utendaji na kuwatumikia kwa ufanisi zaidi wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla.
Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kushinda katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025 ili tuendelee kuongoza nchi kwa uadilifu na ufanisi mkubwa kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazoendana na mahitaji yao ya sasa kiuchumi,kijamii na kimaendeleo",alisema Dkt.Dimwa.
Naye Mkurugenzi mstaafu idara ya umwagiliaji Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt.Ramadhan Aseid Ramadhan,amemshukru Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Dimwa kwa kumjali na kumtembelea kwa dhamira ya kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya Kijamii.
Dkt.Aseid,amempongeza kwa dhati Naibu Katibu Mkuu Dkt.Dimwa kwa utendaji wake unaoleta ufanisi na mabadiliko mkubwa ya kiutendaji ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
04-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
04-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
04-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
04-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
04-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
04-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
04-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
04-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
04-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
04-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
04-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
04-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
04-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
04-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
04-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
04-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
04-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
04-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
04-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
04-12-2025