Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


UFUNGUZI WA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM JIMBO LA MALINDI - ZANZIBAR 

alternative

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Mohammed Said Mohammed 'Dimwa' amesema ni lazima kwa kiongozi wa CCM kuwa na msimamo sahihi wa itikadi katika maisha ya kila siku na kwamba jambo hilo lina umuhimu mkubwa kwa chama hicho.

Dk. Dimwa aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM ya Jimbo la Malindi huko katika Ofisi kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui Mjini Unguja.

Alisema, "ikiwa viongozi hawana itikadi watakuwa si viongozi thabiti kwani Chama Cha Mapinduzi hakiongozwi kwa mabavu bali kwa kuelimisha, kueleza, kushauri, kushawishi na kushirikisha".

Alisema, hiyo ni maana ya kwamba kiongozi wa Chama hana budi kuwa na uwezo wa kushauri, kuelimisha, kushawishi na kushirikisha.

"Huyo ndiyo atakuwa ni kiongozi wetu, na mimi huwa nashangaa sana kwamba anaweza kukaa mtu Mbunge, Mwakilishi au Diwani anakaa miaka mitano lakini hajatuletea hata mwanachama mmoja, hiyo manaake hana uwezo wa kushawishi," alisema.

Alieleza kuwa, Chama Cha Mapinduzi sasa hivi kimegeuaka na kimetoka kwenye analogi na kwamba sasa wameingia kwenye digitali na kwamba hata na uongozi wao wa chini ni lazima aunze kubadilika.

Aidha aliwakumbusha wanachama wa CCM juu ya swala zima la umoja na mshikamano na kwamba hiyo ndiyo silaha kubwa ya Chama hicho.

Pia Dimwa aliwakumbusha viongozi na wanachama wa CCM kutizama mustakabali mzima wa Chama Cha Mapunduzi wapi unapokwenda na kuacha tabia ya kuchukiana bila ya sababu za msingi.

Hivyo aliwaasa viongozi wa Jimbo la Malindi kuacha ugomvi usiokuwa na tija ndani ya chama hicho na kusema kuwa kipindi hiki hakuna sababu yeyote inayopelekea wana CCM kugombana.

Aidha aliwaambia wakati wa uchaguzi utakapofika basi mtu yeyote kwa nafasi yake akiwa ni mwanachama wa CCM na amekidhi haja ya kuwa mwanachama ataruhusiwa kugombea kwa nafasi yeote anayopenda.

"Bahati nzuri sana chama chetu hakina masharti mengi katika kugombea, ikiwa Mwakilishi, Diwani na Mbunge uwe tu unajua kusoma na kuandika tena kiswahili hivyo sifa hizo ni nyepesi sana," alisema

Hivyo aliwataka viongozi na wanachama wa Jimbo hilo kumaliza tofauti zao na magomvi yasiyokuwa na tija na wote lengo lao liwe moja la kukiimarisha Chama cha Mapinduzi.

Sambamba na hayo Dk. Dimwa aliwakumbusha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa ni lazima awe na msimamo wa kijamaa.

Alisema, itikadi ya kiongozi vitendo na tabia yake vinapaswa kujiridhisha kwa kuwaongoza wanachama wa CCM na wa wananchi kwa ujumla kuwa ni vya ujamaa.

Alisema, imani ya kiongozi inaambukiza na kuimarisha imani ya anaowaongoza hivyo kiongozi huyo anapaswa kuwa na vitendo na tabia nzuri kwa wale ambao anawaongoza.

"Lakini kiongozi anayegunduliwa na anayewaongoza kuwa ni mnafiki na kuwa msimamo wake wa uadui ni mkubwa huyo atakuwa ni adui wa Chama chetu," alisema.

Alisema, ameelezwa kuwa katika kikao hicho wajumbe watajadili taarifa za kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kujadili utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi uliofanywa na Mbunge, Mwakilishi na madiwani wa Jimbo la Malindi.

Katika kujadili taarifa hizo aliwaomba wajumbe wa kikao hicho cha Halmashauri kuu ya Jimbo kuzingatia mambo muhimu kwa maslahi ya Jimbo, Chama na Taifa kwa ujumla.

"Taarifa nyingi ambazo zinatolewa nyengine zimekuwa watu wakizipika lakini nyengine siyo za kweli, ila nadhani Jimbo hili la Malindi tunaenda vizuri," alisema

Mahali: Kisiwandui, Zanzibar 
Tarehe : 18 Febuari, 2024

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi