Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Ndg. John V. K. Mongella kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Tume ya Nidhamu na Maadili ya Chama cha Kikomunisti Cha China (CCDI) na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Usimamizi (NCS) ya Serikali ya Watu wa China Ndugu Wang Hongjin.
Aidha katika mazungumzo hayo Mongela aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya China kwa kuendelea kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kwenye nyanja mbalimbali za kiuchumi kwenye Nchi yetu.
Kwa Upande wake Mjumbe wa Kamati ya kudumu ta Tume ya Nidhamu na Maadili ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCDI) na Kamishna wa (NCS) Ndg.Wang Hongjin ameishukuru Serikali ya Tanzania na Chama cha Mapinduzi CCM kwa Ushirikiano mzuri wanaounyesha kwenye suala la uwekezaji na kutoa fursa mbalimbali kwa watu China kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.
Naibu katibu Mkuu Bara amefanya mazungumzo hayo leo tarehe 07.06.2024 kwenye Ofisi Ndogo za CCM Lumbumba Jijini Dar es Salaam.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.