WASIRA AZUNGUMZA NA MAMIA YA WANA CCM MBEYA
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amezungumza na wanachama, viongozi wapenzi wa CCM Mkoa wa Mbeya ambapo amewahakikishia kuwa serikali imedhamiria kufanikisha ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Eden Highland, jijini Mbeya amewataka wananchi waendelee kuiamini CCM na serikali yake ambayo imeendelea kutatua changamoto.