CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar,kimewataka baadhi ya Wananchi kuacha tabia za kuwabagua kwa misingi ya kikabila na kiutamaduni watu wanaotoka katika jamii ya kimasai nchini
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis, wakati akizungumza na Jumuiya ya Wamasai waishio Zanzibar huko Forodhani Jijini Zanzibar.
Mbeto,alisema jamii ya wamasai ni miongoni mwa makabila 120 yaliyopo Tanzania wenye haki ya kuishi popote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata sheria zote za nchi.
Alieleza kuwa sio sahihi baadhi ya wananchi kutumia matukio yaliyotokea hivi karibuni ya ugomvi wa baadhi ya wamasai na maafisa wa Manispaa ya Mjini Zanzibar kuwa ni kigezo cha kuwatenga na kuwakosesha haki zao za msingi,kwani changamoto hiyo imetatuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika maelezo yake,Katibu huyo wa NEC Mbeto,anasema baada ya changamoto hiyo kumejitokeza baadhi ya wananchi na wengine ni watumishi wa umma wamekuwa wakiwakosesha jamii hiyo huduma mbalimbali za kijamii, tabia inayotakiwa kukemewa vikali.
“Chama Cha Mapinduzi kinapiga vita vitendo vya ubaguzi hasa vyenye viashiria vya ukabila kwani madhara yake ni makubwa katika maisha ya kila siku ya jamii zetu na inaweza kusababisha migogoro ya kikabila.
Leo itokee wamasai nao huko kwao Arusha na maeneo mengine ya Tanzania bara waanze kuwabagua na kuwakosesha huduma za kijamii watu wenye asili ya Zanzibar je tutajisikiaje,hatuhitaji kufikia huko kwani sisi ni wamoja na tunatakiwa kuishi kwa upendo na
mshikamano.”alisisitiza Mbeto na kuongeza kuwa ikitokea mtu mmoja au kundi wamefanya uhalifu basi wachukuliwe hao sio jamii yao nzima.
Alisema Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, zote zinaelekeza haki na utu wa kila mtu kuheshimiwa hivyo jamii ya wamasai wasivunjike moyo na waendelee kuishi kwa kulinda amani na utulivu wa nchi.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar italinda haki zao mbalimbali zikiwemo za utamaduni kwani kila jamii ina utamaduni wake utaotakiwa kuthaminiwa kisheria.
Kupitia kikao hicho Mbeto, aliwahakikishia kuwa wamasai wenye sifa za kuwa Wanachama wanakaribishwa kujiunga na CCM na wana haki ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi za Mashina hadi Taifa.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kanda ya Mjini Mathayo Joseph,alisema lengo la kikao hicho ni kutafuta suluhu juu ya changamoto zinazowakabili katika utekelezaji utekelezaji wa majukumu yao.
Alisema kuna baadhi ya maeneo wanapata wakati mgumu kwa kunyanganywa vifaa vyao vya kitamaduni vikiwemo sime na rungu huku wakitolewa kauli zisizofaa zinazowatuhumu kuwa ni wahalifu.
“Miaka yote tumeishi Zanzibar kwa amani na utulivu hatujawahi kuhusishwa wala kukamatwa kwa tukio lolote la kihalifu na mmasai mmoja akifanya kosa ahukumiwe yeye kwani hajatumwa na jamii ya wamasai.”, alifafanua Joseph.
Naye Mwanachama wa Jumuiya hiyo Joseph Olelei,alisema kwa sasa kuna maeneo wanazuiwa kufanya biashara hata kwa wale wanaofanya kazi katika maeneo ya utalii wamewekewa mipaka ya kutofika kwa baadhi ya Pwani kufanya biashara zao.
Olelei amefafanua kuwa wao hawana mgogoro na wananchi wala Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani katika malezi ya jamii yao wamefunzwa kuheshimu jamii zingine na sheria kwa ujumla.
KIPINDI MAALUMU
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
09-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
09-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
09-06-2026
𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀
09-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
09-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
09-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
09-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
09-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
09-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
09-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
09-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
09-06-2026