Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KUTOKULIPA ADA YA UANACHAMA NI KUJINYIMA HAKI YAKO MWENYEWE - NDG. GAVU
> Akemea tabia ya baadhi ya Viongozi kutumia madaraka kujilimbukizia mali
"Ibara ya 16 ya katiba ya chama chetu inaeleza wazi neno kiongozi ya kwamba ni mwanachama aliyepewa dhamana kwa kuchaguliwa au kuteuliwa, sifa kubwa lazima uwe mwanachama na nyenzo na msingi mkubwa ni kuwa mwanachama na ili uwe mwanachama hai yapaswa kulipa ada na kuudhuria vikao."
"Hakuna mwanachama asiyetokana na shina, kila shina lina miongozo na taratibu kwa mujibu wa katiba ya CCM, niwaombe viongozi wetu turudi tukawaambie watu tunaowaongoza umuhimu wa kulipa ada na kushiriki vikao."
"Kutokulipa ada ni kujinyima haki yako mwenyewe ya kuchagua, kuchaguliwa au kutokutana na wenzio."
"CCM tunaona ni jambo la aibu au kashfa kuwa na kiongozi asiyetosheka na hii haimaniishi CCM inapalilia maskini, tunapenda matajiri waliopata utajiri kwa njia za halali na shuguli za halali, kunyanyasa na kuwatenga watu CCM haitakupenda, na matajiri wa kutusaidia ni wale ambao utajiri wao uwe wa halali."
"Kukiwa na kiogozi anayetumia madaraka yake kulimbukiza mali hana sifa ya kuwa kiongozi na Chama chetu na Serikali yetu"
Ndugu. Issa Haji Gavu
Katibu wa NEC - Oganaizesheni wa CCM Taifa
🗓️19 Aprili, 2024
📍Njombe
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.