Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
BALOZI NCHIMBI AONGOZA MAPOKEZI YA KATIBU MKUU, MGOMBEA URAIS WA FRELIMO
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amewaongoza viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, ngazi ya taifa na Mkoa wa Dodoma, kumpokea Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji (FRELIMO), Komredi Daniel Francisco Chapo, ambaye pia ni mgombea urais mteule wa FRELIMO, kwenye Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika mwaka huu mara baada ya kuwasili pamoja na ujumbe wake, katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, leo Jumatano Juni 12, 2024.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.