RAISI WA ZANZIBAR DK HUSSEIN ALI MWINYI AMESEMA SUALA LA MSAADA WA KISHERIA SIO LA ZANZIBAR PEKEE BALI NI LA KIMATAIFA NA LINA HISTORIA KUBWA DUNIANI
Alisema, Zanzibar inawajibu wa kukeleza kwa vitendo huduma za sheria kama lilivyoelezwa kwenye Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 12 pamoja na Sheria nyengine mbalimbali zilizopo nchini. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya nne ya wiki ya msaada wa Sheria, yaliyofanyika ukumbi wa Idrissa Abdul wakili, Kikwajuni Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, watoaji wa msaada wa sheria ni kiungo muhimu cha upatikanaji wa haki nchini hasa kwa wananchi wasio na uwezo wa fedha katika msada wa sheria. Dk. Mwinyi alieleza lengo la kilele cha maadhimisho hayo ni kuzifanya huduma za kisheria kuwa endelevu na zenye kuleta tija kwa jamii sambamba na kutatua changamoto nyengine zinazokwaza huduma za utoaji wa kisheria nchini. Alieleza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora itaendelea kushirikiana na watoa msaada wa kisheria kwa kuhakikisha wanaendelea kutwaa tunzo zaidi, pia wanapata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Pia Dk. Mwinyi alieleza Serikali itahakikisha marekebisho ya Sera na Sheria ya Msaada wa Kisheria yanafanyika kwa ufanisi na haraka ili kukidhi matakwa yanayotakiwa.
Akizungumzia suala la upatikanaji wa vifaa na vitendelea kazi kwa wasaidizi wa wasaidizi wa kutoa msaada wa sheria, Rais Dk. Mwinyi aliwaahidi kwamba seikali inaunga mkono shughuli wanazozifanya b
upatikanaji wa vifaa vya kutendea kazi nayo ni changamoto nyengine. Mazingira wezeshi ya utoaji huduma yanahitaji kuwa na vifaa vya kutosheleza, vikiwemo vyombo vya usafiri, vifaa vya Ofisi kama vile printa, mashine za Fotokopi,
Komputa na kadhalika. Vinapokosekana vifaa hivi, ni dhahiri kuwa daraja la ufikiaji haki nalo hukosekana. Aidha, aliwataka watendaji mbalimbali wa Serikali na taasisi binafsi na vyombo vya kusimamia haki, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Watoaji msaada wa
kisheria ili kuwajengea uwezo wa kufanikisha kazi zao kwa uweledi. Sambamba na kuwaunga mkono na kupata ushirikiano wa kutosha.Hata hivyo alitoa kwa jamii nakuwataka kutimiza wajibu wao kila mmoja kwanafasiyake ili kuwe na mazingira bora ya upatikanaji msaada wa kisheria na kuzidi kuimarisha kiwango cha utawala bora nchini na misingi ya haki za binadamu. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Jaji Mstafu Robert Makaramba alisema, maadhimisho ya 2023 yamekwenda sambmba na mazingira ya uboreshaji wa mifumo, miundo, sera na sheria zinazohakikisha huduma za msaada wa sheria zinatolewa katika hadhi ya zenye lengo la kufikia uwezeshaji wa Serikali kwa kushirikiana na watoa msaada ya kisheria, wadau wa maendeleo, taasisi za kiraia,
wadau wa sekta za haki wakiwemo Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Polisi, Chuo cha Mafunzo na jamii husika.Nae Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Hanifa Ramadhan Said alieleza, watoaji wa msaada wa sheria wanafanya kazi kwa kujitolea na uzalendo kwa uhakikisha wananchi wa Zanzibar wasio na uwezo wanafikiwa na huduma za kisheria kwa sehemu zote ili kutatuliwa haja zao kisheria.
Alisema, maadhimisho hayo walishirikiana na taasisi zote zinazohusu masuala ya sheria, wakiwemo Mahakama, jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Chuo cha Mafunzo na wadau wengine. Maadhimisho hayo ya msaada wa sheria yaliyokuwa na kauli mbiu “Mazingira wezeshi kwa watoa msaada wa kisheria ni daraja la upatikanaji haki” ambayo yalianza Julai 17 na kuadhimishwa Julai 22 mwaka huu yalitanguliwa na shughuli mbalimbali za uhamasishaji ikiwemo kampeni ya vyumbo vya Habari,mkutano na vyombo vya Habari, kutembelea vyombo 21 vya Habari, kufanya program ya vijana kwa Unguja na Pemba, mihadhara na jamii, kufanya usafi wa mazingira kwenye hospitali ya wagonjwa wa Akili, Kidongochekundu, kufanya bonaza na hatimae kuadhimisha kilele halisi wiki ya msaada wa kisheria.
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
22-12-2025
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
22-12-2025
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
22-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
22-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
22-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
22-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
22-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
22-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
22-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
22-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
22-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
22-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
22-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
22-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
22-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
22-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
22-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
22-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
22-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
22-12-2025