Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KINANA AWAHAKIKISHIA WANANCHI HANANGAN MAELEKEZO YA RAIS DK. SAMIA YATATEKELEZWA.

alternative

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wananchi wilayani Hanang Mkoa wa Manyara hususan waliokumbwa na janga la mafuriko, kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu.


Kinana ameyasema hayo leo Desemba 4, 2023 alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.


Kinana amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu zao na waliojeruhiwa na kulazwa hopitalini kutokana na janga hilo ambapo amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
 

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi