Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini katika Ujenzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Maawal Islamiya iliyopo jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa Serikali wa Awamu ya Sita kuunga mkono jitihada za wadau katika kutoa elimu
Kiasi hicho cha fedha kimewasilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akihutubia mamia ya waumini wa kiislamu waliokusanyika kusheherekea kuanzishwa kwa taasisi hiyo na kumbukumbu ya Muanzilishi,Sheikh Shabaani Mohamed Hariri ambapo pia alifikisha salamu kwa waumini hao kutoka kwa Rais Samia huku akigusia kuwepo kwa mporomoko wa maadili unaosababisha uhalifu katika sehemu mbalimbali za nchi.
‘Naomba nitumie fursa hii kuwasilisha salamu za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati nakuja nilimuaga amesema niwasalimie sana na ametoa kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini ikiwa ni mchango wake katika ujenzi wenu wa majengo ya madarasa unaoendelea hapa niwaombe pia mumuombee dua ili aweze kuiongoza nchi yetu kwa salama na amani lakini kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili niwaombe viongozi wa dini muendelee kutumia sehemu zenu za ibada kuiasa jamii iachane na mila na tamaduni ambazo zipo kinyume na mafundisho ya dini zetu’ alisema Waziri Masauni
Wakizungumza wakati wa hafla hiyo,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma,Mustafa Rajab Shabaani na Sheikh wa Mkoa wa Pwani,Alhaji Khamis Mtupa walisisitiza kulindwa kwa maadili katika jamii ambayo yameendelea kuporomoka katika jamii huku wakiwataka waumini kuendelea kuwa karibu na watoto ili kufahamu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
‘Jamii imekumbwa na mabalaa mbalimbali watu wamekua na unyama usiomithilika mpaka imefikia sasa hivi wazazi kuambiwa kuwakagua watoto katika maumbile yao kila wanapotoka shuleni sasa tuitake jamii iwe karibu na watoto ili kuweza kubaini changamoto zao mbalimbali wanazokutana nazo kwani kutokua nao karibu upelekea watoto hao kukumbana na mabalaa lakini kutokuwepo ukaribu kati ya mzazi na mtoto upelekea mtoto kukaa kimya wakati tayari ashaathirika.’alisema Sheikh Mtupa.
Taasisi hiyo ya Maawal Islamiy ina miaka 44 tangu ianzishwe na Sheikh Shabaan Hariri ikijikita zaidi katika kutoa elimu,misaada kwa watu mbalimbali wenye uhitaji na huduma za afya.
🔰𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎!
01-06-2026
𝐒𝐇𝐔𝐋𝐄 𝐘𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐒𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀𝐎𝐍𝐃𝐎𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐌𝐄𝐓𝐀 𝟏𝟐 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀𝐍𝐈 𝐇𝐀𝐈, 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐀𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
𝐍𝐈 𝐌𝐔𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐇𝐀𝐈-𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎 𝐒𝐀𝐒𝐀
01-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐒𝐈𝐇𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐔𝐋𝐄𝐌𝐀𝐕𝐔 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐆𝐔𝐔
01-06-2026
MAWENZI YAVUNJA REKODI: MITUNGI 3,313 YA OKSIJENI YAZALISHWA KWA MIEZI 6, ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 126 ZAOKOLEWA!
01-06-2026
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
01-06-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
01-06-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
01-06-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
01-06-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
01-06-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
01-06-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
01-06-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
01-06-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
01-06-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
01-06-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
01-06-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
01-06-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
01-06-2026