Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, WANA CCM HAKIKISHENI MNALETA WAGOMBEA WAADILIFU, WAPINZANI WANAIFANYA KAZI YAO VIZURI MNO HIVYO MKIWAPA KAZI NYINGINE ITAWASHINDA, NI VIZURI CCM KUENDELEA KUONGOZA NCHI - BALOZI DKT. NCHIMBI

alternative

"Naomba muendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi kuwatumikia, sisi kama CCM tutaendelea kuzisimamia serikali zetu kuhakikisha kwamba kero za wananchi zinatatuliwa kwa wakati na kuhangaika na wananchi wanyonge wa kawaida, kutambua kwamba inao wajibu wa pekee kwa wananchi wetu" 

"Mtakapofika wakati wa uchaguzi serikali za mitaa wana CCM kwa ngazi zote wahakikishe wanatupa wagombea waadilifu , watupe wagombea  wanaoheshimu watu , wapo tayari kutumikia wananchi na ambao tutakapowaletea wagombea hao tunawaomba muwachague wote ili kuendelea kufanya kazi ya kutumikia nchi yetu"

Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amewasihi kuendelea kuiamini CCM katika kuongoza nchi, "Kila watu na kila Taasisi inafanya kazi vizuri katika eneo iliyozoea, kwa mfano fundi cherehani ambaye amekuwa fundi cherehani kwa miaka 15 maana yake ni kwamba uwezo wake wa ufundi cherehani hauwezi kupimanishwa na mtu ambaye hana uzoefu...uongo kweli ? ...na fundi wa ujenzi wa nyumba ambaye amekuwa fundi kwa miaka 40 hawezi kufananishwa na mwengine" 

"Kila mtu anakuwa na ujuzi kwa eneo  ambalo amekuwa anafanyia kazi ...CCM imekuwa madarakani tangu mwaka 1977 ina uzoefu wa kungoza, kuleta maendeleo na imejithibitisha kwa vitendo kwamba inajali maendeleo ya watanzania" 

"Vyama vya upinzani vimekuwepo tangu mwaka 1992 vimethibitisha kwa vitendo kwamba vina uwezo mkubwa wa kufanya kazi ya upinzani kwahiyo muendelee kuwapa heshima hiyo ya kuendelea kuwa wapinzani wetu kwasababu ni kazi wanayoiweza bila mashaka yoyote, wanaifanya vizuri mnoo" 

"Kwakuwa wapinzani wanaifanya kazi yao vizuri mno, mkiwapa kazi nyingine itawashinda kwahiyo kila inapotokea nafasi ya kupiga kura kumbukeni wapinzani ni wazuri kuendelea kuwa wapinzani na CCM ni wazuri kuendelea kuongoza nchi kwahiyo kila taaisis ipeni nafasi kwa udhoefu wake...CCM OYEEE" 

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Mbinga Mkoani Ruvuma.

🗓️22 Aprili, 2024

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi