CCM ITAWALETEA WAGOMBEA SAFI WENYE KIU YA MAENDELEO
Tunajua Mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Sisi ndio tuna Ilani inayotekelezwa, tunaomba Mchague CCM lakini nasisi kama Viongozi Wakuu tutahakikisha tutawaletea Wagombea wazuri na Safi ambao wataenda sambamba na Madiwani na Viongozi wote Katika kuleta Maendeleo. " Wananchi nyinyi tunawajua tukiwaletea mtu mwenye shida mtatuhukumu sasa tunawaahidi watu kuwaletea watu Safi na nitaongea na Wakuu wa Wilaya wote kulisimamia".
Katibu Mwenezi na Mlezi wa Chama Mkoa Dar es salam CPA Amos Makalla amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi na WanaCCM waliofurika Viwanja vya Sekondari Liwiti Jimbo la Segerea ikiwa ni Muendelezo wa Ziara zake kuzungumza na Wana Dar es salam .
🗓08 Julai, 2024